 |
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya cha Uyovu Wilayani Bukombe,Dk Steven Kazuzu akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita,wakati alipofika kushiriki ujenzi wa jengo la upasuaji. |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisaini kwenye kitabu cha wageni ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Bukombe wakati alipowasili |
 |
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Josephat Maganga akisisitiza wananchi kuendelea kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ambazo zinafanywa na serikali ya awamu ya Tano. |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiweka sawa mawe kwenye msingi wa shule ya Sekondari ya Ushirombo wakati alipofika kushiriki na wananchi shughuli za maendeleo. |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na wananchi pamoja na wakina mama ambao wananufaika na mfuko wa TASAF wilaya ya Bukombe. |
 |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe,Safari Mayala akizungumza na wananchi wa uyovu juu ya maendeleo. |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza ushiriki wa wananchi kwenye sekta ya maendeleo kwenye maeneo ambayo wanaishi.
Na,Joel Maduka,Bukombe.
Mila potofu na umbali wa vituo vya afya zimetajwa kuwa kati ya sababu za baadhi
ya wajawazito kujifungulia nyumbani wanapopatwa na uchungu katika Wilaya ya
Bukombe Mkoani Geita.
|
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya
cha Uyovu Wilayani Bukombe Dr Steven Kazuzu alisema uelewa wa wananchi
kuhusu kujifungulia kwenye vituo vya afya ni mdogo na kwamba wengine wamekuwa
na imani potofu kwamba Mwanamke anapojifungulia nyumbani kuna baadhi ya viungo
hubaki navyo tofauti na akijifungulia hospitalini.
“Tatizo kubwa ambalo linasababisha
wakina mama kujifungulia nyumbani ni kuwa na elimu ndogo na kutokujua umuhimu
wa kujifungulia kwenye vituo vya afya na wengine wamekuwa na dhana ya kuwa
hospitali hawezi kupata vitu ambavyo wanavitumia kwenye mambo yao ya
kishirikina hivyo hujikuta wanawalazimisha wakina mama kujifungulia
Nyumbani”Alisema Dr Kazuzu.
Bi,Mery Musa ambaye ni mkazi wa
Uyovu alisema tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu na vifaa kwenye baadhi ya
zahanati hali inayosababisha wengi wao kutoona umuhimu wa kujifungulia kwenye
vituo vya huduma za afya.
Akiwa kwenye ziara wilayani Bukombe,
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alisema lengo la serikali ni
kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa kwa kuwa na majengo ya kutosha na vifaa
tiba pia.
Post A Comment: