MVUTANO mkali umeanza kujitokeza katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya kandanda tanzania bara,baada ya klabu ya wekundu wa msimbazi Simba kuifikia kwa pointi klabu ya Azam FC,kufuatia ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar maarufu kama Mwakata miwa wa mtibwa,katika mchezo uliopigwa jana kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.
Simba ilipata magoli hayo kupitia kwa washambuliaji wake,Ibrahim Hajib aliyefunga goli la kwanza kwa kichwa katika dakika 52 baada ya kona iliyopigwa na Mohamed Husein na kuandikia klabu yake goli la kuongoza.
Kipindi hicho cha pili kilizidi kuwa kigumu kwa Mtibwa kwani katika dakika 66 mshambuliaji aliyesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha Laudit Mavugo akiwa ndani ya 18 akimalizia basi ya mchezaji Mwinyi Kazimoto.
Kwa matokeo hayo yanaiweka Simba katika usukani wa ligi kwa kuwa kufikisha alama 10 ilizozipata baada ya kucheza michezo minne,ikishinda mechi tatu na kutoka sare mechi moja.
VIKOSI:
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Frederick Blagnon dk61, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib/Jamal Mnyate dk75 na Mwinyi Kazimoto/Said Ndemla dk70.
Mtibwa Sugar; Abdallah Makangana, Ally Shomary, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Kevin Friday/Mohammed Juma dk57, Ally Yussuf, Stahmili Mbonde, Ibrahim Juma/Hussein Javu dk73 na Haroun Chanongo.
MATOKEO MENGINE HIYO JANA
Wenyeji Tanzania Prisons walichomoza na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Toto Africas maarufu kama, wana kishamapanda kutoka jijini Mwanza,katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Post A Comment: