Klabu ya African Sports ‘Wana kimanumanu’baada ya kushuka daraja msimu uliopita kwa sasa wamesema kuwa wapo tayari kuanza kwa ligi Daraja la kwanza linalotarajia kuanza Septemba 24,2016 na watakuwa wakitumia uwanja wa Mkwakwani Tanga kama uwanja wao wa nyumbani.
African Sports wamepangwa katika kundi A ambako wanatimu za Lipuli,Mshikamano,Kiluvya,Ashant United,Friends Rangers na Polisi Dar na wataanza ugenini kucheza na Lipuli ya Iringa hivyo wanajipanga kuanza vyema licha ya kuwa Ligi Daraja la Kwanza ni ngumu mno kwani timu nyingi hupania ili ziweze kupata nafasi ya kupanda Ligi kuu ya Vodacom.
Akizungumza na KatangaSports kwa njia ya Simu Katibu Mkuu wa Timu hiyo,Hatibu Enzi,amesema kuwa wana imani watafanya vizuri katika ligi hiyo na wasajili wachezaji 20 na wachezaji wengi waliobaki walikuwa nao kabla ya kushuka daraja japo kuwa kuna wachezaji muhumu wamesajili na timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi kuu ya Vodacom.
‘Tuna jumla ya wachezaji 28 kwani tulifanya kliniki ya kutafuta vipaji kwa wachezaji wadogo ambao tumewasajili na kuungana na wachezaji wetu wa Zamani hivyo tutahakikisha kuwa tutafanya vizuri katika Ligi hiyo na tunaomba wadau mablimbali kujitokeza kuisaidia timu hiyo mchango wa pesa na vifaa mbalimbali ili timu yao iweze kufanya vizuri”alisema Enzi
Aidha amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kusafiri mapema kwenda mkoani Iringa kwani wanatarajia kuondoka tarehe 20 ili kwenda kuzoea hali ya hewa ya huku na kuwa watawafunga wenyeji hao kutokana kuwa walishawahi kuwafunga hivyo mashabiki watengemee kuona timu yao itafanya vizuri hivyo wanatakiwa kusafiri na timu hiyo kwa ajili ya kushangilia.
Post A Comment: