MTEMI MPYA WA DUTWA ASIMIKWA, BARIADI SIMIYU.

Share it:

Ileme John Kasili Mtemi Mpya Dutwa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, akisimikwa rasmi kuwa Mtemi wa eneo hilo na wazee wa kimila pamoja na Watemi wenzake katika Kijiji cha Dutwa kwenye Mti wa Kitemi ulipo kijijini hapo.


Ileme John Kasili (kushoto) akiwa na Mke wake Ngole Kasili, wakisimikwa na wazee wa kimila Kabila la wasukuma, kuwa Viongozi wa Kimila Dutwa wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, zoezi lilifanyikia katika Mti Mkubwa wa kitemi Dutwa.


Mtemi Ileme John Kasili akimwaga maji kuonesha ishara ya kuleta mvua pindi mvua zitakapochelewa katika eneo lake la utawala.


Mtemi wa Dutwa aliyesimikwa Ileme John Kasili (Katikati) akirusha Mshale ikiwa ni ishara ya kupambana na maadui mara baada ya kusimikwa kuwa mtemi, huku akiwa amesindikizwa na wananchi wakiwemo wazee wa kimila.

Ileme John Kasili (Katikati) akiwa na Mke wake Ngole Kasili wakisindikizwa na wananchi wakiwemo wazee wa kimila kutoka nyumbani kwake Dutwa kuelekea eneo la kusimikwa kuwa mtemi rasmi wa eneo hilo

(Picha zote na Derick Milton).



Baada ya Kifo cha aliyekuwa Mtemi wa Dutwa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Paschal Mabiti ambaye pia alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wa Kwanza tangu Mkoa huo kuanzishwa mwaka 2012, Hatimaye jana eneo hilo limepata Mtemi mpya.


Ileme John Kasili ndiye Mtemi mpya wa eneo hilo, ambapo alisimikwa katika eneo maarufu la kusimika watemi wa eneo hilo, eneo la Mti Mkubwa uliko katika kijiji cha Dutwa, kandokando ya Barabara kuu Bariadi-Lamadi, ambapo maelfu ya wananchi wa kijiji hicho walihudhuria sherehe hizo.

Zoezi la kusimkwa kwa Ileme kuwa mtemi mpya wa Dutwa lilianza majira ya saa 4:30 asubuhi nyumbani kwake ambapo alisindikizwa na ngoma za jadi wakiwemo wazee wa kimila, kuelekea katika mti huo na mpaka saa 7:25 zoezi hilo lilimazika hadi kusimikwa, ambapo alipadisha mlimani kwenye e
neo la zahanati ya dutwa ambako mtemi wa zamani ndiko alikoishi.


Baadhi ya wananchi walieleza kuwa kupatika kwa mtemi mpya, ni faraja kubwa sana kwao, ambao walileleza kuwa uwezekano wa kupata mvua kubwa na za kutosha kwa mwaka huu ni mkubwa hali itakayosababisha kupata mavuno mengi.



Share it:

habari

Post A Comment: