RAIS UHURU KENYATTA ATOA MSAADA WA MABATI,MABLANKETI NA MAGODORO KWA WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI

Share it:





Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kuahidi kutoa msaada wa mabati, mablanketi na magodoro kwa wahanga kufuatia tetemeko la ardhi lilioikumba mikoa ya Kanda ya Ziwa juzi Jumamosi, Septemba 10, 2016.


Jana Jumapili, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alimpigia simu Rais Magufuli na kumuelezea majonzi na hudhuni aliyokuwa nayo kwa serikali ya na wananchi wa Tanzania baada ya kusikia taarifa ya vifo vya watu 16 na mamia kujeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba mikoa ya Kanda ya Ziwa (Bukoba-Kagera na Mwanza).


“Nimehudhunika sana kusikia Watanznia 16 wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa pia kuharibiwa vibaya kwa makazi ya watu kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba Wilaya ya Bukoba, Kakazini Mashariki mwa Tanzania” rais Kenyatta alisema.

Aliongeza: “Kwa niaba ya seikali ya na Wananchi wa Kenya, na kwa niaba yangu binafsi napenda kutoa salamu za rambirambi kwa serikali ya Tanzania na familia za wahanga wa tukio hilo.”

Rais Kenyatta anawaombea majeruhi muugue pole na Mwenyezi Mungu awajalie muweze kupona haraka na mrudi kuzisaidia familia zenu na serikali kwa ujumla. Pia anawaombea wafiwa ili Mwenyezi Mungu aendelee kuwatia nguvu na subra hasa katika kipindi hiki kigumu kwao.

Rais Kenyatta amesema, Serikali ya Kenya itatuma msaada wa mabati, mablanketi na magodoro yatakayoletwa Tanzania Jumanne na Jeshi la Ulinzi la Kenya kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko hilo. 

Manoah Esipisu, MBS 

Msemaji Mkuu wa Ikulu, Kenya 

12th September, 2016 
Share it:

habari

Post A Comment: