Mbao Fc wapigwa bao nne kwa Moja katika Dimba la ccm kirumba jijini Mwanza.

Share it:
Mchezo wa Mbeya City  na Mbao FC 
Wachezaji wakiwa katika hali ya kushambulia mpira.




Mashabikiwa wakifatilia machi hiyo.


Mashabiki wa Mbao Fc,wakiwa ahamini kilichotokea.

Kocha wa Mbeya City Kinnah Phiri akiteta na waandishi wa habari.

Kocha wa Mbao Fc,Ettiene Ndairagije,akifafanua juu ya kichapo walichopokea kutoka kwa Mbeya City.


 Na Joel Maduka.

Leo Wakata Miti Wa Jiji La Mwanza Mbao Fc,Wamejikuta Wakiambulia Kichapo Cha Mabao  Manne Yaliyofungwa Na Mbeya City  Huku Wao Wakiambulia Bao  Moja Katika Michuano Ya Ligi Kuu Mchezo Ulichezewa Katika Uwanja Wa Ccm Kirumba Jijini Mwanza.


Mchezo Huo Ambao Umewakutanisha  Mbao FC Na Mbeya City  FC Ulianza Saa 10:00 Jioni Katika Viwanja Vya Ccm Kirumba Huku Timu Zote Mbili Zikionesha Kucheza Mchezo Mkali Hali Ambayo Ilishindwa Kujulikana Ni Nani Ambae Hataibuka Kidedea Katika Ligi Hiyo,Dk Ya 20  Kipindi Cha Kwanza Raphael Daud Aliweza Kuhipatia Gori Moja Mbeya City  ,Mchezo Uliendelea Na Kwenye Dk Ya 34 Mbao Fc Walisawazisha Gori Lililofungwa Na Emmanuel Nchimbi.

Lakini Mambo Bado Yaliendelea Kuwa Magumu Kwa Mbao Fc Ambapo Katika Dk Ya 55 Omary Ramadhani Alifungia Mbeya City Bao La Pili,Gori La Tatu Lilifungwa Na  Ramadhani Chombo Kwenye Dk Ya 75 Na Dk Ya 89 Raphael Chombo Alifunga Bao La Nne,Hadi Mchezo Unamalizika Katika Dimba La Ccm Kirumba Mbeya City Ilikuwa Inaongoza Kwa Mabao Manne  Na Wakata Miti Mbao Fc Wakiambulia Gori Moja.

Kocha Wa Mbao Fc,Ettiene Ndairagije,Alisema Kuwa  Wanamshukuru Mungu Kwa Matokeo Hayo Huku Akikili Kuwa Mbeya City Ni Timu Yenye Uwezo Mzuri Na Kwamba Kwa Sasa Wanajipanga Zaidi Kuweza Kukabiliana Na Mechi Zitakazo Kuja.”Timu Yetu Bado Ni Ndogo Tunaanda Ligi Tunajaribu Waweze Kupata Uzoefu Hivyo Wazidi Kututia Moyo Mashabiki Na Sisi Tunahaidi Kutokuwaangusha Kwa Mechi Zilizobakia”Alisema Ndairagije.

Kwa Upande Wake Kocha Wa Timu Ya Mbeya City Kinnah Phiri,Alisema Kuwa Wao Kama Mbeya City Walikuwa Wamejipanga Vya Kutosha Katika Mapambano Hayo  Hivyo Ushindi Wa Leo Ni Moja Kati Ya Maandalizi Ambayo Wamekuwa Wakifanya Kila Wakati Pindi Wanapokuwa Mazoezini.


Mashabiki Nao Hawakuwa Nyumba Kuzungumza Na J Maduka Blogs ,Ambapo Wamesema Kuwa Timu Zote Ni Nzuri Zilizocheza Leo Lakini Tatizo Ni Tekiniki Zilizotumika Katika Mchezo Huo.
Share it:

matukio

michezo

Post A Comment: