MFUNGWA katika gereza la Wilaya ya Kahama,Shadrack William(32)ambaye ni mkazi wa Ushirombo mkoani Geita,anayetumikia kifungo cha miaka 30 jela,kwa kosa la kulawiti amefikishwa tena Mahakamani kwa tuhuma za kumlawiti Mahabusu wa gereza la mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Akisoma shitaka hilo jipya mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Kahama,Iman Batenzi,Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi,Felix Mbisse,alidai mfungwa huyo;Shadrack alitenda kosa hilo septemba 10 mwaka huu.
Mbisse alisema Shadrack anayetumikia kifungo kwa ajili ya kosa la kulawiti amerudia tena kosa hilo gerezani humo, kinyume cha sheria nambari 154 (1) (a) ya makosa ya jinai sura 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Aidha katika Mahakama hiyo ilimpandisha kizimbani mkazi wa kijiji cha Mbika,Kata ya Ushetu,wilayani Kahama ambaye ni mahabusu katika gereza hilo,kwa tuhuma za kukubali kulawitiwa na Shadrack, ambapo ni kwenda kinyume cha sheria nambari 154 (1) (c) ya makosa ya jinai shitaka ambalo pia amelikana.
Washitakiwa wote wawili wamekana mashitaka dhidi yao hayo yaliyomo kwenye shauri la jinai nambari 547 la 2016 huku mahakama ikiliahirisha shauri hilo hadi Septemba 28,mwaka huu litakapotajwa tena.
Post A Comment: