UVCCM WAWAFARIJI WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI BUKOBA MANISPAA NA MULEBA MKOA WA KAGERA

Share it:
Naibu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu akichangia Damu Kwa ajili ya Majeruhi wa Tetemeko
Shaka Hamdu Shaka ,mwenyekiti wa UVCCM kagera Yahaya (Mwenye tichet aliyechuchumaa ) , katibu wa mkoa UVCCM Kagera Didas Zimbihile (aliyesimama kidogo katikati ) wakisoma dua Kwa moja ya kaburi la marehemu wa janga la tetemeko

Naibu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu akimfariji moja ya wahanga wa tetemeko Mkoani kagera

Shaka Hamdu akiwasili ofisini Kwa Mkuu wa Mkoa Kagera kuwasilisha Msaada wa UVCCM Kwa wahanga

Naibu ,Katibu wa kagera ,Mjumbe wa baraza kuu UVCCM Taifa Mkoa wa Mara Gewa Rashidi (mwenye miwan) wakikabidhi misaada wa mahema pamoja na cement mifuko 100

Hapa akitoa ufafanuzi juu ya msaada waliotoa.


Akitembelea maeneo yaliyo athirika na tetemeko.

Msafara ukiwa ofisin Kwa Mkuu wa mkoa Yaredi Mkuu wa idara ya Chipukizi na hamasa, Naibu Shaka H Shaka ,Mh Waziri kazi Ajira na vijana Jensta Mhagama,Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu.

Umoja wa Vijana wa CCM umewafariji wathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Jumamosi Septemba 10, 2016. Katika msafara uliongozwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) ulijumuisha wajumbe wa baraza kuu Taifa UVCCM,  wajumbe wa Secretariet ya Baadhi ya wajumbe wa  Baraza kuu pamoja na viongozi wandamizi wa UVCCM na CCM Mkoa wa Kagera. 

Kaimu Katibu Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa CCM na jumuiya zake Katika ofisi za CCM Mkoa wa Kagera ambapo alitoa pole na kuwafariji viongozi hao. 

Kaimu Katibu Mkuu alitembelea maeneo  yaliyoathirika na tetemeko hilo na kutoa pole .

Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliwasilisha taarifa ya hali ya maafa na hatua zilizochukuliwa na Serikali mbele ya msafara wa Kaimu Katibu Mkuu .

UVCCM imechangia hema 4 na mifuko 100 ya saruji ambayo Kaimu Katibu Mkuu alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu. 

Kaimu Katibu aliongoza makundi ya Vijana kuchangia damu ili kurudisha damu iliyokuwa imetumika kwa majeruhi toka katika akiba ya damu ya Mkoa wa Kagera. 

UVCCM walifika kukagua madhara yaliyosababishwa na tetemeko hilo katika shule ya Ihungo pamoja na kufika kuhani msiba wa Katibu wa UVCCM kata ya Amgembe manispaa ya Bukoba Marehemu Jonas Bushoke ambae alifariki akiwa katika harakati za kumuokoa mtoto wake. 

Mazungumzo ya Kaimu Katibu Mkuu na Mkuu wa mkoa, viongozi wa CCM mkoa na makundi ya Vijana

Kufuatia malalamiko ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Kagera kulalamikia kitendo kinachofanywa na viongozi wa Chama Cha Demokrasia Maendeleo  (Chadema) kwa kulitumia janga la tetemeko la ardhi kufanya siasa na propaganda potofu.

Uhakiki na utoaji wa msaada katika awamu ya kwanza ulifanyika kwa kuongozwa na vitendo vya ubaguzi na upendeleo huku baadhi ya shehena za mizigo ya misaada na vifaa  vya ujenzi ikiandikwa maneno "ukawa pamoja ".

Kaimu Katibu Mkuu umeitaka na kuishauri  Serikali ni vyema  kuwachia kazi ya uhakiki, ugawaji wa misaada yote kwa waathirika ifanywe na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  (JWTZ) .

Alisema kinachofanywa na chadema ni kituko na fedheha ya kisiasa kuona viongozi wa chama hicho wakilitumia tetemeko hilo kujaribu  kujijenga kisiasa huku kikiwabagua wanachama wa CCM kwa itikadi za kisiasa kinyume na ubinadamu.

Kaimu  Katibu Mkuu alimueleza mkuu wa mkoa Kagera kwamba haitapendeza na dunia itawashangaa watanzania kuwaona baadhi ya watu badala ya kushughulikia majanga na kujali utu  wao wakitafuta sifa za kisiasa.

Pia Shaka alimfahamisha mkuu wa mkoa kwamba katika uhakiki wapo watu wanaomiliki nyumba zaidi ya moja lakini majina yao yanapoonekana zaidi ya mara moja wamekuwa wakisumbuliwa bila sababu 
Mkuu wa Mkoa wa Kagera. 
Akijibu maelezo hayo mkuu wa mkoa Meja Jenerali Kijuu alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itachukua juhudi za kuchunguza na ikithibitika kuwepo kwa madai hayo haitasita kumchukulia yeyote hatua za kisheria .


"Dai hili nitalivalia njuga, vyombo vyetu vikileta taarifa na uthibitisho nitamchukulia yeyote hatua za kisheria, kwanini watu washindwe kutenganisha vipindi vya siasa, wakati wa kazi au wa kukabili majanga na misiba "alisema 

Imeandaliwa na Joel Maduka.
Share it:

magazeti

Post A Comment: