Wafanyabiashara Mkoani Geita wakiwa katika semina. |
Emil Kasagara akifanya utambulisho. |
Meza Kuu kushoto aliyevaa shati la maua ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga na katikati ni Mtendaji Mkuu Wa (BRELA) Frank Kanyusi |
Mtendaji Mkuu Wa BRELA Frank Kanyusi Akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi. |
Wajumbe wa semina wakifatilia kwa makini semina hiyo. |
Mgeni Rasimi ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga Akitoa Hotuba yake katika ufunguzi wa semina hiyo. |
Afisa Mtendaji Wa TCCIA Mkoani Geita Mariam Mkaka,akitoa ufafanuzi juu ya namna ambavyo TCCIA imekuwa ikifanya kazi Mkoani hapo. |
Picha ya pamoja wafanyabiashara na mgeni rasmi Mkoani Geita. |
Picha ya pamoja Mgeni Rasmi na wafanyakazi wa BRELA. |
Kufuatia Ugumu Na Changamoto Ambazo Wafanyabiashara
Walikuwa Wakikutana Nazo Kusafiri Kwa Umbali Mrefu Kwenda Dar es Salaam
Kwaajili Ya Kufuata Usajili Wa Biashara Na Kampuni Wameshukuru
Kwa Wakala Wa Usajili Wa Biashara Na Leseni (BRELA)Kwa Kuweza Kuleta Huduma Ya
Usajili Kwa Wiki Nzima Mkoani Geita.
Kauli Hiyo
Wameisema Mapema Leo Katika Semina
Ambayo Imefanyikia Katika Ukumbi Wa Mikutano Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Geita.
Lengo La
Semina Hiyo Ni Kuwajengea Uwezo Namna
Ambavyo Wafanyabiashara Wadogo Na Wakubwa Wanaweza Kutumia Fursa Ya Kuinua
Vipato Vyao Kwa Kusajili Biashara Na Kampuni Ambazo Wamekuwa Wakifanyia
Shughuli Za Kila Siku.
Raphael
Siyantemi Ni Mfanyabiashara Mkoani Geita,Amesema Kuwa Anaamini Kupitia Semina
Hiyo Ambayo Imeandaliwa Na Brela Itamsaidia Zaidi Namna Ambavyo Anaweza
Kusajili Kampuni Yake.
Nae Bi,Merry
Mpangalala Ameongezea Kuwa Ni Vyema Kwa Brela Wakaona Namna Ambavyo Wanaweza
Kuanzisha Vituo Katika Mikoa Ya Kanda Ya Ziwa Ambayo Itasaidia Kutoa Huduma Ya
Usajili Kwa Urahisi Zaidi.
Aidha Kwa
Upande Wake Afisa Mtendaji Wa TCCIA Mkoani Geita Mariam Mkaka,Ametaja Changamoto Wanazokutana
Nazo Ni Pamoja Na Kurathimisha Majina Kwa Urahisi Kwa Wafanyabiashara Hivyo Wanaamini
ujio wa Brela Mkoani Hapa utatatua
Changomoto Ambazo Zimekuwa Zikiwasumbua Kwa Muda Mrefu.
Kwa Upande
Wake Mtendaji Mkuu Wa Brela Frank Kanyusi, Amesema Kuwa Wamejipanga Kutoa Huduma Zote Za Usajili Kwa Njia Ya Mtandao.
Hata Hivyo
Kwa Upande Wake Mgeni Rasmi Katika Ufunguzi Wa Semina Hiyo ,Mkuu Wa Mkoa Wa
Geita,Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga,Amewashukuru Brela Kwa Kutumia Njia
Ya Kuleta Shughuli Ya Usajili Wa Biashara Kwani Anaamini Itasaidia
Wafanyabiashara Kupunguza Gharama Za Kwenda Dar Es Salaam Kwaajili Ya Usajili.
Imeandaliwa na Joel Maduka
Post A Comment: