Maofisa
mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kwenye makazi ya skari Kigoto
Jijini Mwanza hii leo.
|
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akiwa amembeba mmoja wa watoto
kwenye makazi ya askari Kigoto Jijini Mwanza.
|
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) akisalimiana na maofisa
wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, alipowasili kwenye Gereza la
Butimba Jijini Mwanza hii leo.
|
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) akisalimiana na maofisa
wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, alipowasili kwenye Gereza la
Butimba Jijini Mwanza hii leo.
|
Afisa wa
polisi akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu
Nchemba, kushoto) alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
|
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akizungumza kwenye kikao baina
yake na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la
Butimba Jijini Mwanza hii leo.
|
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akizungumza kwenye kikao baina
yake na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la
Butimba Jijini Mwanza hii leo.
|
Baadhi ya
Maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye kikao
baina yao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba kwenye
Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
|
Wizara ya
Mambo ya Ndani nchini imeahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazovikabili
vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo uhaba wa makazi na sale za askari ili
kufanikisha vyombo hivyo kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa.
Waziri
anayeshughulikia wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, ametoa ahadi hiyo hii leo kwenye
kikao baina yake na viongozi mbalimbali wa vikosi vya Ulinzi na Usalama mkoani
Mwanza, kilichofanyika kwenye gereza kuu la Butimba Jijini Mwanza.
Amesema
jitihada za ujenzi wa nyumba za ghorofa kwa ajili ya makazi ya askari katika
miji mikuu ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam zitaenda sambamba na
ujenzi wa nyumba za kawaida katika wilaya mbalimbali nchini ili kutatua kero
hiyo.
Katika hatua
nyingine, Waziri Nchemba ametoa onyo la kukamatwa wale wote wanaotoa kejeli
kwenye mitandao ya kijamii juu ya utendaji kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama
nchini pamoja na askari wanaopata madhara wakipambana na uhalifu, kama
ilivyotokea katika tukio la mauaji ya askari lililotokea hivi karibuni Jijini
Dar es salaam.
Awali
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, amebainisha baadhi ya
changamoto zinazolikabili jeshi hilo kuwa ni pamoja na ukosefu wa makazi ya
askari, uhaba wa fedha pamoja na madeni ya askari, ambazo zikifanyiwa kazi
zitaboboresha zaidi utendaji wa jeshi hilo.
Kwa hisani ya George Binagi
Post A Comment: