Share it:










Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga,Tarimba Abbas Tarimba,amesema kuwa soka la Tanzania linashindwa kuendelea kutokana na mambo mbalimbali kuanzia kwenye vilabu vyetu na kutokuwa na weledi wa mpira.



Akizungumza na KatangaSports,Tarimba,amefunguka kuwa msingi wa soka ni lazima uanzie kwenye vilabu vya chini pamoja na shirikisho lenyewe na kuanza kufanya mambo kiholela kwani tukiweza kuwa na wachezaji professional kwenye timu zetu tunaamini tutafika mbali.
“Unajua lazima vilabu viwe na wachezaji wenye uwezo wa mkubwa na pia wawe wanatoka mataifa mbalimbali mfano beki wa Yanga,Vicent Bossou yupo kwenye timu ya Taifa na huyu anatoka Afrika Magharibi na wachezaji wengi wa ukanda huo huwa wanaenda ULaya lakini Yeye Yupo Tanzania na timu yake ya Taifa anacheza ni lazima tuwe na misingi imara kwanza kwenye vilabu”alisema Tarimba.

Aidha aliendelea kufunguka kuwa mpira kwa sasa ni biashara na sio ushabiki unahitaji uwekezaji wa hali ya juu tuwe na mifumo ya Hisa ambayo itaweza kuwa na faida kwa kununua wachezaji wenye viwango vya juu wa kushindana na timu za Afrika ya Magharibi na pia itainua soka la nchi kwani makapuni,Taasisi n mashirika binafsi yatawekeza katika soka.
Hata hivyo anamalizia kwa kusema ni lazima vilabu vyetu vibadilike na vikubali kuingia katika mfumo mpya wa kisasa na wenye weledi wa mpira na hii ndio nguzo kubwa ambayo itasaidia vilabu kuwa na uchumi wa kutosha bila kumtegemea mtu na tukifanya hivyo tu naamini soka letu litaimarika kwani wachezaji mbalimbali tena wakubwa kutoka nchi nyingi watakubali kuja kucheza hapa kwetu na kuleta ushindani kwa wachezaji wetu.

Kwa hisani ya Alex Sonna,Dar es salaam.


Share it:

michezo

Post A Comment: