WAZAZI WAPIGWA MARUFUKU KUWARUHUSU WATOTO KUSINDIKIZA HARUSI.

Share it:






NA MAKUNGA PETER MAKUNGA
-

Viongozi wa kata ya sabasabini katika Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama wamepiga marufuku wazazi kuwaruhusu watoto wao kusindikiza harusi hali ambayo imekuwa ikichangia vitendo  vya Ngono wakiwa kwenye sherehe hizo bila ya kujali kwamba watoto hao walikotokea ni wanafunzi wakiwemo wa shule za msingi na sekondari.


Hali hiyo imeelezwa jana na Afisa mtendaji wa kata hiyo Christopher Lyogelo baada ya kumaliza ziara ya pamoja na Diwani wa kata hiyo Emmanuel Makashi kwenye vijiji vya iponyang’holo na Lusonzo baada ya wazazi kukiri kwenye mkutano wa hadhara kwamba baadhi ya wenzao huwaruhusu watoto wao kusindikiza harusi kama desturi ilivyo wakati wa mavuno .

Kufuatia hali hiyo Lyogelo amesema katika mkutano huo wazazi walikubari kutoa ushirikiano na Serikali ya kata hiyo kuhakikisha wanawadhibiti wazazi wenzao watakaobainika kuruhusu watoto wao kusindikiza harusi wakati ni wanafunzi hali ambayo imedaiwa kuchangia mimba kwa wasichana na utoro kwa wavulana.

Hata hivyo Diwani wa kata hiyo Emmanuel Makashi amesema mkakati uliopo ni kuwachukulia hatua kali wazazi watakaobainika kuwakatisha masomo watoto wao baada ya kubaini baadhi ya wazazi kupokea mahali tangulizi za kishika uchumba na kisha kuwarubuni watoto hao wafanye vibaya kwenye mitihani yao ili wakaolewe.

Pamoja na hali hiyo Diwani Makashi katika ziara yake amewataka wanafunzi kuwapuuza wazazi wa aina hiyo ya kuwaharibia maisha badala yake wafanye mitihani kwa kujiamini hasa darasa la saba ambao wameanza kufanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi na kama kuna mzazi atakayebainika kuwarubuni atachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa malengo ya wanafunzi kila shule ni kuwa na ufaulu mzuri.

MWISHO.
Share it:

matukio

Post A Comment: