RAIS MAGUFULI TETEMEKO LA ARDHI LAMZUIA KWENDA ZAMBIA.

Share it:




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara yake ya siku tatu Nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ahudhurie Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu, ili aweze kushughulikia tatizo laTetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16, mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa zimebomoka Mkoania Kagera.

Kufuatia kuahirishwa kwa ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Kumuwakilisha katika Sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika kesho tarehe 13 Septemba, 2016 katika jiji la Lusaka


Jaffar Haniu
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi

Dar es salaam
Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA LIPO IMARA KUDHIBITI UHALIFU NA MAANDAMANO APRILI 26

Jeshi  la polisi mkoani Geita , limewataka  wananchi  katika kuelekea   siku kuu ya pasaka

JOEL MADUKA