|
Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi wa kushoto ni Mwenyekiti wa kanda ya ziwa wa TAMASCA Charles Chacha Wakiwa katika kikao na wamiliki wa makapuni ya ulinzi Wilayani Geita. |
|
Wajumbe wakifatilia kikao kwa makini zaidi wakiwemo kamati ya ulinzi na usalama Wilayani hapo. |
|
Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita ,Herman Kapufi akifatilia kwa makini maoni na ushauri uliokuwa ukitolewa na wakurugenzi wa makapuni ya ulinzi. |
|
Mkurugenzi mtendaji wa umoja Geita SecurityJoseph Mditi akielezea namna ambavyo wanafikilia wao kama wamiliki wa makapuni ya ulinzi wanaweza kutokomeza mauwaji ya walinzi ambayo yamekuwa yakiibuka mara kwa mara. |
|
Mkuu wa polisi Wilaya ya Geita, Ally Kitumbo Akisisitiza namna ambavyo jeshi la polisi wilayani hapo lipo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makapuni ya ulinzi. |
|
Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Geita ,Agwaro Kenedy amesisitiza swala la makapuni kutumia taratibu zinazotakiwa kuwapatia ajira kwa kutumia viongozi wa mitaa. |
|
Kaimu afisa tawala Wilaya ya Geita,Janeth Mobe,akiwashauri wamiliki kudumisha upendo na ushirikiano. |
GEITA:Wilaya ya Geita ni miongoni mwa Wilaya inayokabiliwa na mauwaji
ya walinzi ya mara kwa mara hali ambayo imeendelea kutishia usalama wa baadhi
ya wananchi wanaofanya kazi hizo za ulinzi kuziogopa na mwishowe kujikuta wengi
wanaacha kutokana na kuhofia maisha yao.
Kutokana na hali hiyo imemlazimu Mkuu wa wilaya ya Geita Herman
Kapufi kukutana na wamiliki wa makapuni ya ulinzi yanayofanya kazi
wilayani humo lengo likiwa ni kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili walinzi
katika maeneo yao ya kazi.
Charles Mwita ambaye ni Makamu mwenyekiti wa makapuni ya ulinzi amesema
kwamba ni kipindi kirefu sasa walinzi wameendelea kuuwawa na kwamba swala la
mshahara kuwa mdogo ni sababu ambayo haina mashiko kwani wanachodhani wao
yawezekana kukawa na kikundi ambacho kinafanya mauwaji hayo.
Hata hivyo Kaimu katibu tawala wa wilaya Geita Janeth Mobe
ameomba mashirika hayo kuwa na upendo lakini pia amewashauri Wakurugenzi
kujenga mauhusiano na watumishi waliwaajiri.
“Natambua kuwa upendo ni swala muhimu sana katika shughuli
zetu za kila siku ni vyema kwa makampuni ya ulinzi kuwa na upendo lakini pia ni
muhimu kuwa karibu na wafanyakazi ambao mnawaajiri unakuta Mkurugenzi wengine
hajawahi kukutana hata siku moja na wafanyakazi wake hali ambayo inapelekea
kushindwa kujua shida za wale uliwaajiri”alisema Mobe
Aidha kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi
amewaagiza wamiliki wa makampuni kuwa na walinzi ambao wanakuwa na afya njema
lakini pia wawe wamepitia mafunzo ya mgambo, na pia ameagiza mikesha yoyote ya
kidini pamoja na kumbi za starehe
kuhakikisha wanakuwa na vibali na wanafunga kwa wakati sahihi maeneo ambayo
wanafanyia biashara na yale ambayo wamekuwa wakiendesha ibada ili kudhibiti
uharifu ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara.
Imeandaliwa na Joel Maduka.
Post A Comment: