Baada ya kufungwa magoli matatu
na Brazil hatimaye Leo timu ya Argentina wameibuka na ushindi wa magoli
3-0 dhidi ya Colombia mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Estadio De
Bicentenario wa kuwania nafasi ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2018
nchini Urusi.
Argentina walikuwa wa kwanza
kupata goli kupitia kwa nahodha na mchezaji wa kutengemea wa klabu ya
Barcelona Lionel Messi dakika ya 10 akifunga goli safi akitumia udhaifu
wa mabeki wa Colombia na kuwanyanyua mashabiki wa Argentina waliofurika
katika uwanja huo.
Lucas Pratto aliifungia tena
Argentina magoli mawili ya haraka haraka katika dakika za 23 na 28 na
kuwafanya Colombia wapotee kwa kuchanganikiwa na hayo magoli matatu hadi
timu zinaenda mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa magoli matatu kwa
bila.
Kipindi cha pili kilikuwa kigumu
kwa kila timu kwani zilishindwa kufungana na Colombia wakishindwa hata
kupata goli la kufutia machozi hadi mwamuzi toka nchini Eduardor
,Zambrano anamaliza mpira Argentina wameibuka na ushindi wa magoli 3-0
na kuwapandisha juu ya msimamo.
Sasa Argentina imepanda hadi
nafasi ya tano wakiwa na pointi 19 huku Colombia nao wakishuka chini
nafasi ya sita wakiwa na pointi 18 na matokeo mengine,Eduador 3-0
Venezuela,Chile 3-1 Uruaguay,Peru 0-2 Brazil.
VIKOSI:
Argentina: Romero;
Mercado, Otamendi, Funes Mori, Mas; Mascherano, Biglia; Di Maria (Acuna
85′), Banega (Perez 63′), Messi; Pratto (Higuain 79′)
Subs: Roncaglia, Rulli, Guzman, Pizarro, Demichelis, Correa, Zabaleta, Belluschi, Aguero.
Goals: Messi, Pratto.
Booked: Funes Mori, Mercado, Banega, Pratto
Colombia: Ospina;
Arias, Sanchez, Murillo, Balanta; Sanchez, Cuadrado, Torres (Copete
67′), Barrios (Torres 46′), Rodriguez; Falcao (Bacca 76′)
Subs: Cardona, Perez, Gonzalez, Muriel, Vargas, Medina, Borja, Diaz, Aguillar.
Booked: Alvarez, Arias, Rodriguez, Cuadrado
Post A Comment: