![]() |
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilombero 1 kata ya Lwamgasa Wilayani Geita ,Bw Mahano Bitendo Bihogo akiwa nje ya mahakama kabla ya kusomewa mashitaka ambayo yalikuwa yakimkabiri. |
![]() |
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilombero 1 kata ya Lwamgasa Wilayani Geita ,Bw Mahano Bitendo Bihogo ,akiingia ndani ya mahakama kwaajili ya kusikiliza mashitaka ambayo yalikuwa yakimkabili. |
![]() |
Mwendesha mashitaka wa Takukuru ,Bw Kelvin Murusuri akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ambazo zimechukuliwa mahakamani dhidi ya mwenyekiti wa Kilombero 1. |
![]() |
Mkuu wa Takukuru Mkoani Geita,Bw Thobias Ndaro,akitoa ufafanuzi juu ya hatua ambazo wameendelea kuzichukua dhidi ya watu ambao wamekuwa wakiendekeza vitendo vya Rushwa Mkoani humo. |
Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Geita imemuukumu Mwenyekiti wa kijiji cha Kilombero
1,Bw Mahano Bitendo Bihogo kwenda jela miaka mitatu kutokana na kukutwa na
hatia ya makosa matatu ambayo ni
kushawishi na kupokea hongo kinyume na kifungu cha 15(1)(a)na(2)cha sheria ya
kuzuia na kupambana na rushwa na kosa la kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu cha sheria na kanuni za adhabu sura ya 16 R:E 2002.Katika shauri la
jinai Na.114/2018.
Akisoma hukumu hiyo mbele ya
mwendesha mashitaka wa Takukuru ,Bw Kelvin Murusuri
Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Geita,Kaliho Mrisho amesema mahakama
imemkutana na hatatia mshitakiwa na
kwamba mahakama imejiridhisha pasipokuwa na shaka yoyote na ushahidi ulioelezwa
na mwendesha mashitaka ,Bw Murusuri baada ya mtuhumiwa kukiri kutenda makosa
hayo.
Mwendesha mashitaka wa Takukuru Bw,Kelvin Murusuri
amesema mwenyekiti huyo Aliomba
na kupokea fedha kiasi cha milioni moja kutoka kwa mwekezaji Hussein Mwananyanzara ili awapatie posho wajumbe wa serikali ya
kijiji kwa lengo la kukaa kikao ambacho
kililenga kumjadili na kumpitisha kuendelea na shughuli zake.
Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mshitakiwa alipewa nafasi ya
kujitetea kabla ya kutolewa adhabu
alijitetea kuwa anao watoto na mke na wote wanamtegemea ,kutokana na utetezi huo mahakama ilimpa adhabu ya
kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya laki tano kwa kila kosa na kwa
makosa yote alitakiwa kulipa milioni moja na nusu ,Mwendesha Mashitaka hadi
anaondoka mahakamani mtuhumiwa alikuwa ajalipa faini hiyo na amepelekwa
gerezani.
Mkuu wa Takukuru Mkoani Geita,Bw Thobias Ndaro ametoa wito
kwa wananchi wa mkoa huo kuendelea kufichua uonevu na kushiriki vyema kwenye
mapambano dhidi ya vitendo hivyo kwa kutoa taarifa mbali mbali za vitendo vya
rushwa katika Nyanja zote ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria
na kwa kufanya hivyo wananchi watakuwa wameshiriki kutokomeza vitenndo vya
Rushwa.
Post A Comment: