![]() |
Mzee John Mkubila akiwa ameshikiliwa na Moja kati ya wananchi ambao wanaishi mtaa wa Mwembeni Kata ya Nyankumbu Mjini Geita baada ya kukamatwa ameoa binti wa miaka kumi na tatu(13). |
![]() |
Mzee John Mkubila akizungumza juu ya suala la kumuoa Binti wa miaka kumi na tatu wakati alipokuwa amekamatwa na jeshi la polisi jamii. |
![]() |
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo akizungumza juu ya hatua ambazo zimechukuliwa na jeshi la Polisi kutokana na tukio la mzee John Mkubila.
Jeshi la Polisi Mkoani Geita Linamshikilia Mzee wa miaka sitini na tisa (69) kwa kosa la kumuoa Binti
wa Miaka kumi na tatu(13) ambaye
anatokea kitongoji cha Rwenge Kijiji cha Bugalama.
Mzee huyo ambaye anajulikana kwa jina la John
Mkubila ambaye ni mkazi wa mtaa wa mwembeni kata ya Nyankumbu mjini Geita
amekiri kumuoa binti huyo kwa makubaliano ya mzazi wa binti huyo kuwa awe anamsaidia kazi za
nyumbani kutokana na mke wake kuwa na majukumu mengi ya kibiashara hali ambayo
imepelekea kujikuta mzee akikosa huduma
za msingi na kuamua kumuoa binti huyo.
“Nilionana na Baba yake nikamwambia kuwa kwa sasa
umri wangu umekwenda naweza kupata binti mdogo wa kunisaidia maana kwangu nina
mke ila ana majukumu mengi hivyo najikuta nashindwa kufanya shughuli zingine
Baba yake akaniambia sawa ndio akawa amenipa huyu ambaye kwa sasa ni Mke
Mdogo”Alisema Mzee Mkubila.
Aidha kwa upande wa Binti huyo amekiri kuolewa na
mzee huyo kutokana na na
Baba yake mzazi kumlazimisha.
“Mimi nilikataa kuolewa Baba yangu ndiye ambaye
alinilazimisha niolewe kutokana na kwamba
nimemaliza shule ya msingi ila mimi sikuwa tayari kuolewa kutokana na
umri wangu kuwa mdogo”Alisema Binti.
Hata hivyo kwa baadhi ya wananchi ambao walikuwa
wamejitokeza kwenye ofisi za polisi jamii kwenye mtaa huo wamesikitishwa na
kitendo hicho na kuitaka jamii kubadilika na kuachana na desturi ambazo
zimeendelea kuwakandamiza watoto wa kike .
Kamanda wa Polisi Mkoani Humo Mponjoli
Mwabulambo amesema nyuma ya tukio
kulikuwa na mapatano baina ya wazazi wa mtoto na huyo mzee kama mahari ilitolewa lakini pia uchunguzi
unafanyika na utakapokamilika wote watafikishwa mahakamani kwa kuwa ni kosa la
kisheria kujamiana na mtoto mwenye umri
wa chini ya miaka kumi na tano(15).
|
Post A Comment: