 |
Madawati yaliyotolewa na Shwekelela |
 |
Pankalas Shwekelela akielezea namna ambavyo wameguswa kusapoti madawati katika halmashauri ya mji wa Geita. |
 |
Shwekelela na mke wake wakifurahia baada ya kuwa wamekabidhi madawati kwa mkuu wa wilaya ya Geita. |
 |
Wanafunzi wa shule ya msingi kalangalala wakifurahia baada ya kupatiwa madawati. |
 |
Afisa Elimu Msingi,Catherin Mashala akielezea changamoto ambazo zipo katika wilaya hiyo kwa upande wa elimu. |
 |
Mkuu wa wilaya Mwl Herman Kapufi akitoa maagizo kwa wanafunzi kuakikisha wanaunza madawati hayo ili yaje yawafae kwa baadae. |
 |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akikabidhi madawati kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Mji pamoja na baadhi ya wanafunzi. |
 |
Wanafunzi Elizabeth John wa shule ya msingi kalangalala akitoa shukrani baada ya kukabidhiwa madawati hayo kwenye shule yao. |
 |
Mkuu wa wilaya akimshukuru Bw,Shwekelela na mke wake kwa kuguswa kuchangia maendeleo ya elimu wilayani hapo.
|
GEITA:Jamii
na Mashirika wilayani Geita,yameombwa kuendelea kujitolea kuchangia madawati
ili kunusuru wanafunzi kuendelea kukaa chini pindi wanapokuwa masomoni.
Rai
hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi wakati alipokuwa
akikabidhiwa madawati 14 yaliyotolewa na
familia ya ndugu Shokelera.
Amesema
kuwa wanafunzi walioandikishwa ni wengi
sana kwenye wilaya hiyo hivyo wengi
wamejikuta wakikaa chini na kurundikana madarasani na kushindwa kuelewa kile
ambacho wanafundisha pindi wanapokuwa madarasani huku akiwataka wale wote
waliotoa ahadi kutekeleza kile walichoahidi.
“Nitoe
wito kwa wananchi wa Geita ambao wanajua kwamba tuna watoto wengi sana tuna wanafunzi
wengi sana bado tunahitaji madawati waendelee kujitolea”Alisema Kapufi
Aidha
kwa upande wake,afisa elimu msingi,Halmashauri ya mji ,Bi Catherin Mashala,ameelezea
kuwa madawati hayo kumi na nne (14) ambayo yametolewa yatapelekwa shule ya
msingi Kalangalala iliyopo wilayani hapa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi
kukaa chini.
Kwa
upande wake Panklas Shokerela,amesema kuwa wametoa madawati hayo kwa lengo la
kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk John Magufuli ya
kuhakikisha wanaondokana na changamoto ya watoto kuendelea kukaa chini, na
kwamba wataendelea kuchangia mambo mbali mbali katika swala la elimu.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Apolinary,amewashukuru wadahu
ambao wameendelea kujitolea kuchangia madawati katika halmshauri hiyo.
Imeandaliwa na Maduka online blogs.
Post A Comment: