Akisisitiza juu ya kutokukataza mikesha makanisani kwani anatambua kuwa ni moja wapo ya ibada ambazo zimekuwa zikifanyika kuombea Taifa pia. |
Wachungaji na maaskofu wakimwombea mkuu wa wilaya ili Mungu haendelee kumsaidia katika shughuli za kulijenga Taifa pamoja na wilaya ya Geita. |
Baadhi ya watumishi wa Mungu wakifatilia kile ambacho kilikuwa kikielezwa na Mkuu wa wilaya ya Geita. |
Mwenyekiti wa CPCT ambae pia ni Askofu wa kanisa la FPCT Mkoani Geita,David Nzumbi akimshukuru mkuu wa wilaya kuhuzulia katika kikao chao na kutoa ufafanuazi juu ya katazo la kutokukesha usiku. |
Wakiombea Taifa pamoja na Rais John Magufuli katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku. |
Katibu wa CPCT Mkoa wa Geita,Mch Joshua William akimweleza mkuu wa wilaya juu ya adha ambazo wamekuwa wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na kurazimishwa kujiunga na jeshi la jadi la Sungusungu. |
GEITA:Baraza
la Makanisa ya kipentekoste wilaya ya Geita ,limemwomba Mkuu wa wilaya hiyo kushughulikia katazo la kukesha
lililotolewa mnamo Oktoba 19 lililokuwa likizuia mikesha makanisani kwa
vigezo vya Ulinzi na Usalama.
Akinukuu katiba
ya nchi ibara ya 19 kipengele cha 1 na 4 ambacho kinatoa haki na uhuru wa
kuabudu bila ya kuvunja sheria ya nchi katika kikao cha baraza hilo na mkuu wa wilaya
katibu wa baraza hilo, Mch Joshua Willium ,amesema kuwa wao pia ni wadawu wa swala zima la amani na
wanatambua misingi ya amani katika Taifa.
“Mh,Mkuu wa
wilaya tunaamini wewe ni Mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika wilaya na pia
sisi ni wadau wa amani katika wilaya ,Mkoa na hata Taifa pia tunaomba utusaidie
kulishughulikia jambo hili linalotaka kutugawa kwa kutuonyesha kwamba Serikali
yetu haipo pamoja nasi,jambo ambalo siyo kweli kwani hata Rais wetu anatusisitiza tuombe na kumwombea”Alisisitiza
Joshua
Kwa Upande
wake mchungaji Robert Ngai amesikitishwa na tabia za baadhi ya askari wa jeshi
la Sungusungu kwenye Tarafa ya Busanda kuwalazimisha
watumishi wa Mungu ambao ni wachungaji kujiunga
na Jeshi la jadi la Sungusungu huku imani zao zikiwakatalia kujiingiza katika maswala ya jadi swala hili
amemwomba mkuu wa Wilaya kulishughulikia.
Akijibu
maombi hayo ambayo ameombwa na baraza hilo kupitia kwa viongozi Mkuu wa wilaya
ya Geita,Herman Kapufi amefafanua kuwa yeye hana tatizo na watumishi wa Mungu
wala maswala ya mikesha kwani anaamini kuwa ni watu ambao wanaliombea taifa
huku akiwataka kutoa taarifa za kupatiwa ulinzi pindi wanapokuwa kwenye mikesha
wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani na kuahaidi kushughulikia swala
la wachungaji kuombwa kucheza sungusungu.
Imeandaliwa na Madukaonline blogs.
Post A Comment: