GEITA:WANAWAKE WAPANGIWA SIKU ZA KUJIFUNGUA.

Share it:
Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema Upendo Peneza akiwaelezea wananchi kushikamana nan kuwa kitu kimoja ili kupinga swala la kupatiwa Miamba taka(Mangwangala)katika kijiji cha nyakabale kilichopo wilaya na Mkoa wa Geita.

Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema Upendo Peneza,akijaribu kuteta jambo na Mwenyekiti wa kijiji cha Nyakabale  juu ya matatizo ambayo yamekuwa yakikikumba kijiji hicho.

Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema Upendo Peneza,akiwatunza fedha kwa kuimba vizuri kwaya ya kijiji cha nyakabale

Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema Upendo Peneza,akiselebuka kwa furuha na wanakwaya ambao walimvutia uwimbaji wao.

Msemaji wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema,Deogratias Shinyanga.akiwaeleza wananchi namna ambavyo wanaweza kutoa ushirikiano katika kutatua kero na changamoto ambazo zimekuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu.

Katibu wa Mbunge Shida Mpondi akimkaribisha mbunge kuzungumza na wananchi ambao walikuwa wamekusanyika kwaajili ya kusikia kile ambacho wameitiwa ikiwa ni pamoja na kuelezea kero ambazo zinawakabili kijijini hapo.

Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa hadhara  wakimsikiliza mbunge kwa umakini juu ya kile ambacho alikuwa akikizungumza .



Wananchi wakiunga hoja ya kupatiwa maeneo ya uchimbaji na kuachana na mangwangala ambayo yameonekana kutokuwa na dhahabu.

Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema Upendo Peneza,akifatilia kwa makini hoja za wananchi zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.

Mzee ,Kennedy Nyakikelege ,akielezea kusikitishwa kwake na maeneo ambayo yamewekewa bikoni na mgodi wa dhahabu wa GGM.



Bi,Agnes Peter akielezea masikitiko yake kwa niaba ya wanawake katika kijiji cha nyakabale kutokana na kupangiwa siku za kujifungua.



Wanawake katika kijiji cha nyakabale kata ya Mgusu wilaya na Mkoa wa Geita,wamewalalamikia baadhi ya wahudumu wa zahanati ya kijiji hicho  kwa kuwapa siku za kujifungua  ambapo  siku ya jumamosi na jumapili huduma hiyo inasitishwa kwa madai kuwa ni siku za mapumziko.

Hayo wameyasema kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema Upendo Peneza kijijini hapo,ambapo wamesemakuwa kumekuwa na kero ya watumishi kupanga siku za mama wajawazito kujifungua katika zahanati hiyo jambo ambalo linahatarisha maisha ya wajawazito wengi.

wamesema kuwa uongozi wa zahanati hiyo ulipanga siku tano za wanawake kujifungua na siku mbili za jumamosi ni siku za watumishi kupumzika na kuacha maswali kwa wananchi juu ya wanawake wanaopatwa na uchungu siku hizo kwani hawana sehemu nyingine na kuwalazimu kusafiri mpaka katika hospitali ya Mkoa

Kutokana na maelezo ambayo yalitolewa na akinamama hawa ,swala ili limemsikitisha mbunge wa viti maalum,Upendo Peneza na kuahaidi  kufikisha madai yao kwa mkurugenzi wa halmashari ya mji wa geita kupata ufumbuzi wa jambo hili.
“Nimesikitishwa sana tabia ambayo wakina mama wamekuwa wakifanyiwa kwa kupangiwa siku ya kujifungua mimi mama yangu alinizaa siku ya jumamosi ina maana ningepangiwa siku ya kuzaliwa nisingekuwepo duniani hili swala kamwe hatuwezi kulivumilia nitahakikisha ninafikisha malalamiko haya kwa ngazi usika”Alifafanua Upendo

Madukaonline imemtafuta mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Dkt, Deogratias Digala, ambapo amekanusha  tuhuma hizo na kusema kuwa muda wowote na siku yoyote huwa wanazalisha na hayo madai ni kwamba hayana ukweli ndani yake kwani tabia ya kijiji kuwachongea watumishi kwa viongozi ni jambo ambalo limekuwa nila mara kwa mara.

Sanjali na hayo Mh,Peneza amewaomba wananchi kuungana kwa pamoja kuomba maeneo ya uchimbaji na kuachana na dhana ya kuendelea kugombea miambataka maarufu kwa jina la magwangala.

Imeandaliwa na Madukaonline.



Share it:

habari

Post A Comment: