Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Mkoa wa Geita, Dkt Vito Kajoba ,Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu swala la lishe ambavyo limekuwa likisababisha magonjwa ya kisukari na presha. |
Wananchi waliojitokeza kwenye huduma ya kupima wakisubilia huduma ya kupima afya katika Hosptary ya rufaa ya Geita. |
Huduma ya upimaji ikiendelea . |
Afisa tawala wa wilaya ya Geita,Saashisha Mafuwe,akiwasisitaza wananchi kujenga desturi ya kupima mara kwa mara na pindi wanaposikia huduma hiyo inatolewa Bure |
Dokta Bingwa wa magonjwa ya kisukari Wilayani Geita,Joseph Makuma akielezea hali ilivyo kwa ugonjwa huo Mkoani Geita. |
Ulaji wa
kupindukia na vyakula vyenye wanga na
mafuta ni sababu ambayo imeelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa magonjwa ya
kisukari na presha.
Hayo
yameelezwa na mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Mkoa wa Geita, Dkt Vito Kajoba
wakati wa zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza lililofanyika katika
hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.
Amesema kuwa
kutokana na dhana ambayo imejengeka kwa wananchi wengi kula vyakula vyenye
mafuta mengi na kutokuwa na mpangilio wa ulaji ni sababu moja wapo ambayo
imekuwa ikisababisha kuwepo kwa magonjwa
ya kisukari na presha, na hivyo ameshauri ili kuepukana na magonjwa hayo ni vyema kwa jamii kujenga desturi ya
kufanya mazoezi mara kwa mara.
“Tuchukue
hatua zifuatazo kwanza turekebishe lishe vyakula vyetu vya mafuta na vyenye
wanga mwingi tutumie kidogo sana lakini pia tufanye mazoezi ili kupunguza
mafuta ambayo yanakuwa yamerundikana mwilini”Alisisitiza Kajoba
Kwa upande
wake afisa tawala wa wilaya ya Geita,Saashisha Mafuwe,amewasisitaza wananchi
kujenga desturi ya kupima mara kwa mara na pindi wanaposikia huduma hiyo
inatolewa Bure ni vyema wakajitokeza kwa wingi kuangalia afya zao.
Hata hivyo
kwa upande wao wananchi ambao walikuwa wamejitokeza katika zoezi la upimaji
wameishukuru Serikali huku wakiomba huduma hiyo kupelekwa na maeneo ya vijijini.
Pamoja na
zoezi la upimaji wa magonjwa
yasiyoambukiza bado wananchi wanakabiliwa na changamoto ya kutopata dawa na
huduma za kiafya pindi wanapokuwa wameathirika.
Post A Comment: