Wanafunzi wakipata picha ya pamoja na mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa GGM
Jumla ya madawati elfu mbili (2) yametolewa katika wilaya ya Geita, na kampuni ya
uchimbaji wa Madini ya dhahabu ya Geita(GGM) lengo likiwa
ni kutatua changamoto za wanafunzi kuendelea kukaa chini na kubanana pindi
wanapokuwa darasani.
Akizungumza katika zoezi la kukabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa wilaya ya Geita,Meneja
mwandamizi wa maswala ya jamii,Manase Ndoroma, amesema kuwa wametoa madawati hayo kama sehemu ya kuimarisha elimu kwenye jamii na mahitaji makubwa kwa sasa hivi
katika jamii ni swala la kupunguza watoto kukaa chini hali ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.
“Tumetoa madawati haya kama sehemu ya mchango wetu wa kuimarisha elimu
katika jamii tunajua kwa sasa hivi mahitaji makubwa katika jamii ni kuwepo kwa
madawati”Alisema Manase
Aidha kwa upande wake Afisa elimu msingi halmashauri ya mji wa Geita Bi,
Catherin Mashala ameelezea kuwa sekta ya elimu inakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa madawati hivyo kupelekea baadhi
ya wanafunzi kukaa chini, na kuongeza
kuwa wilaya ya geita ina jumla ya wanafunzi
laki 2,24,350 na hivyo kwa kanuni za kielimu wanahitaji madawati elfu 80,770 na
madawati yaliyopo ni elfu 47,123
upungufu ni elfu 33,839
Wanafunzi wa shule ya msingi mseto, Gedion Joseph na Eva
Johanes wameishukuru kampuni ya GGM kwa kuweza kujitoka kusaidia swala la elimu
na pia wameahaidi kuendelea kuyatunza madawati
hayo ili yaje yawasaidie wanafunzi wengine ambao watakuja kuyatumia.
Mgeni rasmi katika shughuli ya makabidhiano ambae ni mkuu wa wilaya ya
Geita,Mwl Herman Kapufi, amewataka wanafunzi na walimu
kutunza madawati ambayo watu binafisi na makapuni yamekuwa yakijitoa ili yaje yawe msaada kwa wanafunzi wengine
Kampuni ya dhahabu ya GGM ,imekwisha kusaidia swala la elimu kwa kujenga
shule ya kisasa ya Sekondari ya wasichana ya Nyankumbu,maktaba,pamoja na
kurekebisha shule zilizoezuliwa na kuchangia madawati Mkoani Geita.
Imeandaliwa na Madukaonline
|
Post A Comment: