![]() |
Muonekano wa nyumba zilizezuliwa na Mvua iliyonyesha usiku wa tarehe 1 November |
Nyumba zipatazo 236 kata ya Ilyamchele wilayani Chato zimeezuliwa na mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali usiku wa tarehe 1 Novemba, 2016.
Mvua hiyo pia imeezua jengo la mahabara ya sekondari ya kata ya Ilyamchele, ofisi ya kata na kijiji, kanisa la AICT Ilyamchele,nyumba ya mwalimu,nyumba ya muuguzi,ghara la pamba na mazao yanayokadiriwa kuwa hekali 113 yameharibiwa vibaya.
Hakuna vifo ila watu 28 wamejeruhiwa na mmoja amevunjika mguu. Hadi sasa kaya 38 hazina mahali pa kuishi. Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Shaaban Ntarambe tayari amefika eneo la Tukio ambapo amewashukuru wananchi waliojitolea kuwapa hifadhi kaya 38 ambazo nyumba zao zimeharibika kabisa yaani hawana mahali pa kuishi huku akimwagiza mhandisi wa ujenzi kuweka kambi katika eneo hilo ili kuhakikisha miundombinu yote iliyoharibika hasa ile ya umma inarekebishwa mara moja na kuendelea kutoa huduma.lakini pia kawashauri kila kaya kupanda miti kwani kuna ukataji wa miti mkubwa eneo hilo
Imeandaliwa na Afisa habari wilaya ya Chato
Post A Comment: