Sengerema. Tabia ya wanaume wilayani hapa, Mkoa wa Mwanza kuuza
mazao yakiwa shambani au yaliyohifadhiwa nyumbani bila kuwashirikisha
wenzi wao imedaiwa kuchangia umaskini na njaa.
Imeelezwa asilimia 56 ya kaya wilayani hapa zinakabiliwa na umaskini na njaa kila mwaka kutokana na vitendo hivyo.
Hayo yalibainika wakati wa mdahalo ulioandaliwa na shirika lisilo la
kiserikali la Kivulini kujadili changamoto zinazosababisha umasikini wa
kipato na njaa miongoni mwa wakazi wilayani hapa.
Mkurugenzi wa shirika hilo, Yassin Ally alisema utafiti kuhusu umaskini
wa kipato na tatizo la njaa kwa Sengerema umebaini familia nyingi hupata
mavuno ya kutosha kutokana na kilimo cha mahindi na mpunga, lakini
mazao hayo huuzwa na wanaume yakiwa shambani au baada ya kuvunwa na
kuhifadhiwa nyumbani.
Navigation
Post A Comment: