Waziri wa Afya, Maeendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na wauguzi hawapo
pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha
kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha
leo Mkoa wa Pwani.
Waziri wa Afya, Maeendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria
uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi
na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Waziri wa Afya, Maeendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiweka udongo
kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza
wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa
wa Pwani.
Waziri wa Afya, Maeendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia michoro ya jengo
litakavyokua pindi litakapomalizika wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi
katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini
lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Baraza la Wauguzi na Wajunga
nchini wametakiwa kutowaonea aibu wale wote wanaoanzisha vyuo vya afya
kama mradi wa kujiingizia fedha bila ya kuwa na taaluma hiyo kwani
kunapelekea kuhatarisha Maisha na afya za watanzania.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati
akiweka jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na
wakunga kitaaluma nchini lililopo mjini kibaha Pwani.
“Hatusemi wasianzishe vyuo,bali
vyuo vyote viwe vyenye hadhi ya kutoa wataalam stahili ,visajiliwe na
vikaguliwe mara kwa mara ili vizalishe wauguzi wenye sifa na ujuzi
stahili,uuguzi siyo ujasiliamali,hakikisheni mnavifungia vyuo vyote feki
ili tuweze kudhibiti utitiri huu” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy alisema hivi
sasa kumekuwepo na utitiri wa vyuo vingi vya uuguzi ambavyo
havijasajiliwa na havizalishi wauguzi ambao wanastahili kuajiriwa kwenye
sekta ya afya na hivyo kuhakikisha wanasimamia taaluma hiyo na
kuvifungia mara moja vyuo vilivyokosa sifa.
Waziri Ummy alisema kuwa serikali
inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na wauguzi katika
hospitali zote nchini hivyo maboresho yatafanyika na kuhakikisha
upatikanaji wa vitendea kazi kwa wauguzi.
“Asilimia 80 za kazi zote katika
hospitali zetu nchini zinafanywa na wauguzi na wakunga hivyo Serikali
imesikia kilio chenu na tutahakikisha tatizo hili tunalitatua” alisema
Ummy.
Hata hivyo Waziri Ummy aliwataka
wauguzi kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia maadili na viapo vyao vya
kitaaluma kwa maendeleo ya Afya nchini.
Kwa upande wa Msajili wa Baraza
la Uuguzi na Ukunga nchini Bi. Lena Mfalila alisema jengo hilo
linajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza limegharimu pesa ya
kitanzania shilingi bilioni 2.2.
Aidha Bi. Mfalila alisema kuwa
ujenzi wa kituo hicho ulianza Desemba 2015 kwa awamu ya kwanza na
kiinatarajiwa kukamililika na kuanza matumizi yake Januari2017 .
Post A Comment: