Mchungaji wa kanisa la Last church of God Mkoani Geita,Ezekiel Mayala akiongoza ibada ya uzinduzi wa Kiwanda kidogo cha kukoboa mpunga cha Kaboja katika sherehe za uzinduzi. |
Baadhi ya wageni waalikwa katika shughuli ya uzinduzi wa kiwanda hicho wakifatilia kile ambacho kilikuwa kikiendelea. |
Wakurugenzi wa kiwanda hicho,Bw &Bi Emmanuel Kaboja wakiwakaribisha wageni waalikwa kwenye shughuli ya uzinduzi. |
Mitambo ya kukoboresha Mpunga na kupembua ikiwa bado hijazinduliwa |
Diwani wa kata ya Buhala hala ,Mussa Kabese ambae alikuwa ndie mgeni rasimi kwenye uzinduzi huo akikata utepe kuhashiria kuwa amekwisha kukizindua kiwanda hicho kufanya kazi. |
Mkurugenzi wa Kaboja Rice Mill,Emmanuel Kaboja akikagua mashine hizo pamoja na mgeni rasmi. |
Diwani Mussa Kabese akiwasha mashine ili kujua kama mitambo inafanya kazi kwa ufasaha. |
Hapa akiangalia namna inavyokoboa mpunga mashine hiyo. |
Baadhi ya wananchi wakiangalia mitambo ya kukoboa mpunga. |
Diwani Musa Kabese akisisitiza jamii Mkoani Geita ,kuchangamkia fursa zilizopo Mkoani humo na kuchana na dhana ya kujua dhahabu ndio fursa pekee. |
GEITA:Wananchi
wilayani na mkoani Geita,wametakiwa kutumia fursa ambazo bado hazijafikiwa na
watu wengine ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika viwanda vidogo ili kujikwamua
katika janga la ukosefu wa ajira.
Wito
huo umetolewa na diwani wa kata ya Buhalahala , Mussa Kabese wakati wa uzinduzi
wa kiwanda kidogo cha kukoboa
mpunga cha
Kaboja kilichopo eneo la mwatulole.
Amesema
kuwa ni vyema kwa wananchi kuwa na mtazamo tofauti na kwamba fursa pekee sio
dhahabu tu katika mkoa wa Geita kwani bado kuna mambo mengi ya msingi ambayo
yanaweza kuleta faida na kutoa ajira kwa vijana ambao hawana ajira.
“Kumekuwepo
na dhana kwa wananchi mkoani Geita hata kwenye kata ninayoiongoza ya Buhalahala
kuona kwamba fursa pekee iliyopo Mkoani hapa ni madini ya dhahabu tu kumbe sio
kweli kuna fursa nyingi sana leo tumeona mwezetu Kaboja ameweka mashine ya
kisasa ya kukobolesha mpunga na naamini ataajiri vijana hivyo atakuwa amesaidia
swala la upungufu wa ajira nchini niombe wananchi kuwa na mawazo nje ya box kwa
kuziona fursa na kuzitumia kama ilivyo kwa maeneo mengine”alisema Kabese.
Kwa
upande wake ,mkurugenzi wa kiwanda hicho Emmanuel Kaboja,ameelezea kuwa lengo lake la kufungua kiwanda hicho
kidogo cha kukoboa mpunga ni kutoa ajira kwa watanzania ikiwa ni pamoja na kuongeza
pato la Taifa.
“Mimi
ni mfanyabiashara wa mashine kwa muda mrefu nilianzia mashine ya kukoboa na
kusaga mahindi na kusambaza unga wa sembe lakini mtaji ulipokuwa nimeona ni
vyema nikafungua mashine hii ya kukoboa
mpunga ambayo nina amini itatoa fursa kwa baadhi ya vijana kuajiliwa hapa na
kuinua kipato kwa Taifa na familia”alifafanua Kaboja.
Aidha
kwa upande wake bi,Rebeca Emmanuel ambae ni mke wa mkurugenzi wa kiwanda hicho ,amewashauri
wakina mama kuwa na ushauri mzuri kwa wanaume katika swala la maendeleo hili kujinasua kutoka katika hali
ya utegemezi katika familia zao.
“Natambua
Kuwa mwanamke anamchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya mwanaume niwaombe
wanawake wenzangu wawe tayari kuwashauri wanaume kubuni miradi ambayo italeta
faida kwa akina baba na familia kwa ujumla”alisema Rebeca.
Imeandaliwa na madukaonline blogs
Post A Comment: