Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo akizungumza na waandishi wa habari juu ya matukio hayo. |
Watu wawili
wameuwawa kwa nyakati tofauti Mkoani Geita,ambapo tukio la kwanza lilitokea Novemba
6 katika kijiji cha magiri kata ya Kasenga Wilaya ya Chato,tukio linguine limetokea
kijiji cha Buyagu kata ya Nyakamwaga,tarafa ya Busanda wilaya ya Geita,ambapo
mwanaume alimuua mke wake na kitu cha ncha kali kwa kile kinachoelezwa ni wivu
wa mapenzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoani Geita,Mponjoli
Mwabulambo amewataja waliuoawa ni Lucia Yagalaza(43)Mkazi wa Buyagu, shughuli
ni Mkulima na Ndilachuza Kengere(80)mkazi wa kijiji cha magiri, shughuli ni
mkulima.
Amesema
tukio la kwanza ambalo lilitokea tarehe sita ambalo liliondoa uhai wa
Ndilachuza Kengere marehemu akiwa nyumbani kwake sebuleni aliuwawa na watu wasiofahamika kwa kunyongwa hadi kufa kwa kutumia kamba ya
chandarua na kisha kupakwa unga usoni na watu hao kutokomea kusikojulikana.
Jeshi la
Polisi linaendelea na msako mkali ili kubaini kiini cha tukio hilo na
kuwatafuta wale ambao wameusika na kifo hicho.
Kamanda
Mponjoli,ameendela kuelezea kuwa tarehe 8,Lucia Yagalaza(43) aliuawa na mume
wake aitwaye Charles Isamwile kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani
akiwa amelala kitandani,mara baada ya kufanya mauaji hayo mtuhumiwa alienda
kuwaaga watoto wao ambao walikuwa wamelala nyumba nyingine kuwa anasafiri
ingawa hakusema anakwenda wapi wala hakuwataarifu kuhusu kuuawa kwa mama yao.
Kamanda
ameongezea kuwa uchunguzi wa kina unaonesha kuwa chanzo cha tukio ni ugomvi wa
kifamilia uliotokana na marehemu kumtuhumu mtumiwa kuuza shamba lao bila ya
kumshirikisha ,katika eneo la tukio kulikuwa na shoka ambalo lilikuwa na damu
ambalo linasadikika kutumika katika mauaji hayo.
Mtuhumiwa
amekwisha kukamatwa na yupo mahabusu muda wowote atapandishwa kizimbani kujibu
mashitaka yanayomkabili.
Kamanda
ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kwamba
kama kuna mambo ambayo ni mazito ni bora wakafika kwenye vyombo vya sheria ili
kupatiwa msaada wa kisheria.
Imeandaliwa na Madukaonline Blogs
Post A Comment: