DC GEITA KUFANYA SENSA YA WAGANGA WA JADI.

Share it:
Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi akizungumza na wananchi wa kata ya Bukoli wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya wakati alipokuwa akitoa maagizo.



Mkuu  wa wilaya ya Geita  Mwl Herman Kapufi amesema hatasita kuwasaka na kuwakamata waganga wajadi wanaopiga ramli chonganishi na kusababisha mauji ya vikongwe na walinzi kwenye Wilaya hiyo.

 Kauli hiyo  ameitoa wakati wa ziara ya kikazi kwenye kata ya Bukoli iliyopo wilayani Geita alipokuwa akizungumza na wananchi juu ya mikakati ya kuinua kilimo cha Pamba wilayani humo.

Kapufi amesema kuwa  anatarajia kufanya sensa mwakani ya kubaini waganga wa jadi waliopo katika wilaya ambayo anahiongoza na kutoa vibari kwa upya lengo likiwa ni kubaini na kujua wale ambao wamekuwa wakifanya shughuli hizo kinyume na taratibu zilizopo kwasasa.

Aidha ameongeza kuwa  anatarajia kufanya ziara kwa kila kijiji na kata kwa kuzungumza na wazee hili kubaini chanzo cha mauaji yanaoendelea kwa walinzi na vikongwe.

Maduka online imezungumza na Mwenyekiti wa chama cha waganga Mkoa wa Geita Bujukano Maungu amesema Mkoa wa Geita una waganga wa jadi 7800 lakini wenye sifa za kutibu wakiwa awafiki 200 huku mwenyekiti wilaya Zakaria Kanyenye akisema watendaji wengi wanakwamisha zoezi la ukamataji.

Wilaya ya Geita inaongoza kwa kuwa na matukio mengi ya mauaji ya walinzi na vikongwe kati ya Wilaya tano zilizoko ndani ya Mkoa huo jambo ambolo linadaiwa waganga wa jadi wasiokua na sifa ndio chanzo.
Share it:

habari

Post A Comment: