Kibanda ambacho amekutwa mtu huyo akiwa amehifadhiwa baada ya mauaji |
Baadhi ya wananchi wakiwa katika hali ya mshangao |
Zikiwa ni siku nne tangu mlinzi mmoja ambaye anajulikana kwa jina la Michael Williamu (28) Mkazi wa Ngorongoro Mkoani Manyara kuchinjwa kisha kuuwawa na watu wasiofamika wakati akiwa kwenye Rindo lake mtaa wa msalala Road kata ya kalangalala mtu mwingine ambaye akufaamika mara moja jina lake wara makazi yake amechinjwa na mwili wake kutupwa kwenye boma ambalo alijaisha.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea juzi majira ya saa kumi na mbili asubuhi katika mtaa wa nendeni na amani kata ya Buhalahala Wilaya na Mkoa wa Geita.
Wakizungumza na maduka online iliofika katika eneo la tukio baadhi ya mashuuda wamesema kuwa mtu huyo ambaye akufaamika mara moja amekutwa akiwa amechinjwa na mwili wake kutupwa ndani ya boma ambalo alijaisha huku jina lake likishindwa kujulikana kwa mapema zaidi
Diwani wa kata hiyo Musa Kabese amesema kuwa wamejipanga kukabiliana na swala hilo huku afisa tarafa Ahamad Hussein akisema wameandaa utaratibu kwa watu wanaoingia kwenye mitaa na kata hizo kusajili majina yao na kujiandikisha lengo likiwa ni kulinda ulinzi na usalama katika maeneo hayo.
Jeshi la polisi Mkoani hapa limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea kubaini chanzo chake.
Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi akizungumza kwa njia ya simu amewataka wananchi kuendelea kushilikina kwenye swala la ulinzi kwani ni jukumu la kila mtu.
Kwa upande wake Askofu wa kanisa la T.A.G jimbo la Geita Saimon Masungu ameomba serikali kuanza kuwasaka waganga wanaopiga ramli chonganishi na kusababisha maujia.
Matukio ya kuchinjwa kwa watu na walinzi katika Mkoa wa Geita yanazidi kupamba moto jambo ambalo baadhi yao wananchi wanaoingia na kutoka wameakuwa wakiogopa.
Post A Comment: