|
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani
Geita Iddi Kassim Iddi,akiendesha Harambee ya umaliziaji wa ujenzi wa madarasa kwenye kanisa la AIC Kalangalala. |
|
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani
Geita Iddi Kassim Iddi pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita ambaye pia ni muumini wa kanisa hilo,Leornad Kiganga Bugomola wakifurahia kwa pamoja wakati wa harambee. |
|
Mjumbe wa SINODI na Mwenyekiti wa idara ya vijana wa kanisa la AIC Kalangalala wakicheza kwa pamoja wakati wa zoezi la uchangiaji wa harambee ya umaliziaji ujenzi wa madarasa ya watoto. |
|
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani
Geita Iddi Kassim Iddi,na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita Leonard Bugomola wakiwa kwenye harambee. |
|
Mchungaji wa kanisa la AIC Kalangalala John Masanyiwa pamoja na mama wakipandisha ngazi kwaajili ya kwenda kutoa mchango wao. |
|
Mchungaji Johh Masanyiwa akitoa mchang wake pamoja na mama mchungaji. |
|
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita Leonard Bugomola akibadilishana mawazo na katibu wa UVCCM Mkoa wa Geita. |
|
MNEC Iddi Kassim akipokea zawadi ya kitenge kutoka kwaya ya vijana Geita. |
|
Mzee Yohana Madundo akiwa na kuku ambaye alipigwa mnada kwaajili ya kupatikana fedha ambazo zinaelekezwa kwenye ujenzi wa madarasa. |
|
MC Jonathan Masele akiongoza zoezi la mnada wakati wa harambee ya ujenzi wa madarasa. |
|
Kikundi cha kusifu na kuabudu. |
|
Mwenyekiti wa idara ya wanawake kanisa la AIC Kalangalala,Bi,Agnes Kamagi akishukuru kanisa kwa kuweza kujitoa kwenye harambee ya umaliziaji ujenzi wa madarasa ya watoto. |
|
Mch,John Masanyiwa akisoma kiasi ambacho kimepatikana kwenye harambee hiyo ya kanisa. |
|
Mch,John Masanyiwa akielezea namna ambavyo ujenzi ulianza mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi mkoani Geita Iddi Kassim. |
|
Madarasa ambayo yamejengwa kwaajili ya watoto wa kanisa la AIC Kalangalala. |
|
Mgeni Rasmi pamoja na mchungaji na viongozi wa kanisa la AIC Kalangalala wakikagua baadhi ya majengo ambayo yamekwishakujengwa. |
|
Mchungaji ,John Masanyiwa akitoa maelezo ya namna ambavyo ujenzi unaendelea Kwasasa.
Na,Joel Maduka,Geita.
|
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani
Geita Iddi Kassim Iddi,amefanikisha upatikanaji wa kiasi cha shilingi milioni
13.2 ,mifuko ya seruji 70 na mabanti ya kisasa 131 kwaajili ya ujenzi wa
madarasa ya watoto kwenye kanisa la AIC Kalangalala Wilayani Geita.
MNEC wa mkoa huo Iddi ameendesha harambee hiyo siku ya leo
kwenye ibada ambayo ilikuwa imeandaliwa na idara ya wanawake wa kanisa la AIC Kalangalala kwaajili ya
changizo la umaliziaji wa madarasa ya kujifunzia watoto kanisani hapo.
Akisoma risala mbele ya
mgeni rasmi kwa niaba ya watoto wa
kanisa hilo,Bi Justina Yuda ameeleza mahitaji ya ujenzi wa madarasa ya watoto kwa awamu ya pili
yanatarajia kugharimu kiasi cha Tsh
19,185,000 na kwamba fedha hiyo itasaidia kuezeka,kuweka dali kwenye madarasa pamoja na kuweka frame za madirisha
,milango na mageti ya milango.
Katika harambee hiyo MNEC Iddi milioni 1 papo hapo,mifuko 20 ya
seruji na mabati 13 huku akitumia nafasi hiyo kuendesha harambee ambayo iliweza
kusaidia kupatikana kiasi cha sh,milioni 12.2 hivyo kupelekea kupatikana kwa
jumla ya kiasi cha sh,milioni 13.2 ambazo zitatumika kujenga madarasa ya
kujifunzi watoto.
Akihutubia
mamia ya waumini hao Mara baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimia waumini wa kanisa
hilo MNEC Iddi aliwasisitiza waumini hao
kuendelea kuunga jitihada za uchangiaji wa madarasa pamoja na ujenzi hili
kuweza kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwakabili wanafunzi wengi kwa
sasa.
Pia amewaomba kundelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya
awamu ya inayooongozwa na kusimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe.
Dkt John Pombe Magufuli kwani imejipambanua kuwanufaisha wananchi kupitia
rasilimali zao.
Aliwasihi
waumini hao kuiombea serikali ya Rais Magufuli sambamba na wateule na watumishi
wake wote ili waendelee kuliongoza Taifa na sekta mbalimbali katika ushirika
mwema wakiongozwa na roho mtakatifu kila mmoja kwa imani yake.
Aidha kwa upande wake
mchungaji wa kanisa hilo John Masanyiwa alisema kukamilika kwa madarasa hayo matatu yatawasaidia watoto kuweza kujifunza
katika vipindi vya ibada na pia kwa upande wa idara ya wanawake yatawasaidia
kuwa kama kitega uchumi kwa maana ya kukodisha kwaajili ya shughuli mbali mbali
zikiwemo za semina na warsha ambazo zitakuwa zikifanyika.
Pia,Mch Masanyiwa
amemshukuru MNEC wa mkoa wa Geita kwa kufanikisha shughuli ya harambee hiyo.
Post A Comment: