Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita akizungumza na waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wakati wa ibada, leo 3 Machi 2017.
Waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe akizungumza wakati wa ibada mara baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, leo 4 Machi 2017.
Waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombeakizungumza wakati wa ibada mara baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, leo 4 Machi 2017.
Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita akikabidhiwa kitabu cha mara baada ya kuzungumza na waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe wakati wa ibada, leo 4 Machi 2017.
Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita akifanyiwa maombi na mchungaji Lazaro Mbogo wa kanisa la waadventisti Wasabato Maganzo kwa ajili ya utendaji uliotukuka kwa kusimamia haki na wajibu mara baada ya kuzungumza na waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe wakati wa ibada, leo 4 Machi 2017.
Na Mathias Canal, Geita
Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita amefanikisha upatinaji wa jumla ya shilingi milioni 4.6 kwa ajili ya ununuzi Wa Vifaa vya muziki kwa ajili ya kwaya ya Maganzo katika kanisa la Waadventisti Wasabato.
Mhe Biteko ameendesha harambee hiyo 3Machi 2018 katika ibada ya kawaida ya juma kwa mujibu wa utaratibu wa kanisa hilo aliposhiriki ibada maalumu ambapo pamoja na mambo mengine waumini wa kanisa hilo walimuomba kuchangia ununuzi Wa Vifaa vya kwaya hiyo kwa ajili ya kuendeleza utumishi wa kuhubiri injili kwa njia ya uimbaji.
Katika harambee hiyo Mhe Biteko alichangia shilingi milioni 2 papo hapo huku akitumia nafasi hiyo kuendesha harambee ambayo ilipelekea kupatikana shilingi milioni 2.6 hivyo kupelekea kwaya hiyo kupata jumla ya shilingi milioni 4.6 huku uhitaji wa ununuzi wa Vifaa hivyo vya muziki nukiwa ni shilingi milioni 10.
Akihutubia mamia ya waumini hao Mara baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimia waumini Wa kanisa hilo Mhe Biteko alisisitiza kuwa wananchi kwa ujumla wake wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayooongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwani imejipambanua kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali zao.
Aliongeza kuwa katika sekta ya Madini ambapo ndiyo Wizara aliyopewa jukumu ya kuiongoza Mhe Biteko alisisitiza kuwa Rais Magufuli amedhamiria kurejesha uchumi fungamanishi kwa wananchi hususani kuwainua kwa kuwalea wachimba wadogo hatimaye kufikia uchimbaji wa kati na hatimaye baadae kuwa wachimbaji wakubwa.
Aliwasihi waumini hao kuiombea serikali ya Rais Magufuli sambamba na wateule na watumishi wake wote ili waendelee kuliongoza Taifa na sekta mbalimbali katika ushirika mwema wakiongozwa na roho mtakatifu kila mmoja kwa imani yake.
Alisema kufanya hivyo ni kulinufaisha Taifa kwani watendaji wengi wanafanya kazi kwa weledi lakini majukumu hayo yamekuwa na lawama nyingi kwani usimamizi wa sheria hauwezi kumfurahisha kila mtu lakini Taifa lolote ili liendelee ni lazima kuwe na usimamizi madhubuti wa sheria na taratibu za nchi.
Alisema kuwa wananchi wa Tanzania wamezaliwa katika nchi ambayo inautajiri wa kila aina kwa kuwa na Rasilimali nyingi yakiwemo Madini mengi lakini ilisalia kuwa nchi nufaishi kwa wageni kuliko wazawa.
Hivyo utashi wa serikali ya awamu ya tano ni kuwainua wananchi wanyonge ambao kwa muda mwingi walipoteza matumaini katika kipindi kirefu pasina fikra za mafanikio.
Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko leo 4 Machi 2018 ameanza ziara ya siku nne katika Jimbo lake la Uchaguzi (Bukombe) Mkoani Geita itakayofika ukomo 6 Machi 2018 ambapo pamoja na mambo mengine atakutana na wapiga kura wake ili kusikiliza matatizo yanayowakabili ikiwa ni pamoja na kuyatafutia ufumbuzi.
Post A Comment: