Jengo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya chato likiendelea kujengwa. |
Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo Rajabu Mfinanga,akitoa maelezo juu ya ujenzi huku akionesha baadhi ya vyumba na kazi ambazo zitakuwa zikifanyika katika vyumba hivyo. |
Kaimu mganga mfawidhi wa hosptali ya wilaya ya chato,Joelam Mpemba,akielezea changamoto zilizopo kwa sasa hosptalini hapo kutokana na uhaba wa vyumba vya upasuaji mbele ya waandishi wa habari. |
Mgodi
wa dhahabu wa Geita,GGM umefadhili kiasi cha sh,Milioni miatatu thelathini na
tano (335) kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji wilaya ya Chato Mkoani
Geita.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliofika na kujionea ujenzi ambao unaendelea katika jengo
hilo la upasuaji Meneja mwandamizi wa
maswala ya jamii wa GGM Manase Ndoroma alisema
kuwa Chato ni moja kati ya wilaya ambazo zipo kwenye mkoa wa Geita na ndio
sababu ambayo imepelekea kutoa fedha kwa
ajili ya ujenzi wa jengo hilo.
“Chato
ni moja ya wilaya za mkoa wa Geita ambapo tunafanyia shughuli zetu na tunu yetu
kubwa ni kuona eneo ambalo tunafanyia kazi zetu watu wanafaidika na uwepo wetu
katika suala la maendeleo ya jamii na ndio maana tumeamua kufadhili kiasi cha
sh,milioni miatatu thelathini na tano (335) za ujenzi wa jengo la upasuaji
ujenzi umefanyika kwa kiwango kikubwa na wa kisasa zaidi kama ambavyo
tumejionea”Alisema Manase
Kwa
upande wake msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo Rajabu Mfinanga,ameeleza kuwa
jengo hilo lina sehemu za upasuaji mbili
(2) na kwamba litakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji kwa watu watatu (3) kwa
wakati mmoja hali ambayo itasaidia kuondoa foleni ya watu wanaofanyiwa upasuaji
kama ilivyo kwa sasa.
Kaimu
mganga mfawidhi wa hosptali ya wilaya ya chato,Joelam Mpemba amefafanua kuwa
jambo kubwa ambalo liliwaladhimu kuomba ufadhili wa kujengewa jengo hilo ni
kutokana na wingi wa watu ambao wamekuwa wakija katika huduma ya upasuaji na
kwamba sehemu ya upasuaji iliyopo kwa sasa ni ndogo kwani imekuwa ikibeba mtu
mmoja .
“Kilichosukuma
kuomba kujengewa chumba cha upasuaji ni kulingana na mahitaji tuliyonayo kwa
siku tunaweza kupasua wagonjwa watano na kwa sasa tunahudumia baadhi ya wilaya
kama Muleba na Biharamulo kwa maana hiyo mahitaji ni makubwa kuliko ilivyokuwa
kwa zamani”alifafanua Mpemba
Aidha
kwa upande wa wananchi ambao walikuwa kwenye matibabu Hosptalini hapo wamesema
kuwa kukamilika kwa ujenzi huo utasaidia kupatiwa huduma ambayo itakuwa ni
nzuri zaidi.
Imeandaliwa na Madukaonline.
Post A Comment: