Mkurugenzi
wa tume ya uchaguzi nchini Ramadhani
Kailima,akitoa taarifa ya uchaguzi mdogo kwa waandishi wa habari katika ofisi ya mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Mkoani Geita.
|
Baadhi ya waandishi wa habari wakimfatilia kwa makini,Mkurugenzi
wa tume ya uchaguzi nchini Ramadhani
Kailima wakati alipokuwa akitoa taarifa. |
Wajumbe kutoka tume ya uchaguzi wakisikiliza taarifa ya uchaguzi mdogo. |
Uchaguzi mdogo wa Mbunge wa Jimbo la Dimani, wilaya ya Mjini Magharibi na madiwani katika kata 22 nchini, utafanyika Januari 22 mwakani ambapo uchukuaji fomu utaanza Jumamosi ijayo.
Uteuzi wa wagombea utafanyika Desemba 22 mwaka huu huku kampeni zikianza Desemba 23 hadi Januari 21 mwakani.
Akitoa Taarifa ya uchaguzi Mkoani Geita kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi nchini Ramadhani Kailima.
Alisema Mbunge wa Jimbo hilo, Tahir Ali Hafidh alifariki Novemba 11, mwaka huu mjini Dodoma alikokuwa katika mkutano wa Bunge baada ya kuugua ghafla. Alisema pia wataendesha uchaguzi mdogo kwa nafasi 22 za Udiwani zilizoachwa wazi kwa sababu mbalimbali kwa baadhi ya halmashauri za Tanzania Bara.
Alizitaja kata hizo na mikoa ziliko kwenye mabano kuwa ni Ng’hambi na Ihumwa (Dodoma), Kiwanja cha Ndege (Morogoro) Igambavanu, Ikweha (Iringa), Ngarenanyuki na Mateves (Arusha), Kijichi (Dar es Salaam), Kinampundu (Singida), Isagehe (Shinyanga) na Kasansa (Katavi).
Nyingine ni Malya na Kahumulo (Mwanza), Maguu na Tanga (Ruvuma), Kamwani (Kagera), Nkome (Geita), Lembeni (Kilimanjaro), Mkoma (Mara), Duru (Manyara), Mwamtani (Simiyu) na Misugusugu (Pwani).
Kailima
ameongeza kuwa kwa wale ambao wamepoteza vitambulisho vya kupigia kura na
wale ambao wamefikia umri awatapiga kura
hadi pale utakapofika muda wa kuboresha taarifa katika daftari la wapiga kura.
Hata hivyo
ametumia fursa hiyo kuviasa vyama vya siasa ,wadau wa uchaguzi na watendaji
wote watakaoteuliwa kuwa wasimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Dimani na kata
kuzingatia sheria,kanuni,maadili,miongozo na maelekezo yote ya halali yaliyopo
yonayosimamia uchaguzi.
Imeandaliwa na Madukaonline.
Post A Comment: