Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi aliyechomwa Mkuki na wafugaji wa kwanza kushoto. |
Kwanza
niruhusu nikupe Pole ndugu yangu kwa lililokukuta. La msingi Serikali
inatakiwa kujua, tunaposema maoni yetu pale Bungeni tunamaanisha. yako
mambo unaweza yafanyia utani lakini hapa tulipofika si kwa kuchukulia
mzahamzaha.
Waziri
muhusika haya hauyaoni au niliposimulia juu ya Wananchi wa Jimbo la
Chalinze kupigwa , kuvunjwa migongo na mwengine kupigwa mshale wa goti
na kumpa ulemavu wa maisha mlidhani natania. Sasa hili liwe fundisho.
Serikali ni lazima ije na majibu sahihi juu ya kunusuru vita ya wenyewe
kwa wenyewe .
Jana
mtu kavunjwa mgongo, mwengine mlemavu leo kapigwa mkuki wa mdomo
umetokea shingoni. Lini tutasikia kilio hiki? Serikali sikieni kabla
Damu ya watanzania wanyonge wanaotegemea kilimo kama kiinua mgongo chao
hawajapotea. Kuna sheria, na mipango ya matumizi bora ya Ardhi. Nini
kinafichwa?
Binafsi
Nalaani Vitendo hivi na kuiasa Serikali yangu kujipanga vizuri kabla
mambo hayajaharibika. yalianza Kilosa, Mvomelo, Chalinze, Handeni,Kiteto
na sasa Mikumi ( kutaja maeneo machache) .Serikali jipangeni, kabla
hapajachafuka.
RIDHIWANI KIKWETE
MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE.
Post A Comment: