Waziri wa TAMISEMI,Simbachawene akipokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa madarasa shule ya msingi Bomba mbili nyuma yake ni Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu,pamoja na diwani wa Buhala hala Mussa Kabese.
Wakurugenzi na wenyeviti
wa Halmashauri ya wameonywa kuacha kuchezea na kutumia
isivyotakiwa fedha za ruzuku zilizotengwa na serikali kwaajili ya shughuli za
maendeleo ya wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George
Simbachawane wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa
madarasa na vyoo vya shule za msingi pamoja na kuweka jiwa la msingi pamoja na
kuzindua majengo hayo Katika wilaya na Mkoa wa Geita.
Waziri Simbachawene alisema
serikali haitawavummilia viongozi hao
wa ngazi za halmashauri watakaobainika
wametumia fedha hizo kinyume na taratibu ambazo zimepangwa.
alisema kuwa anazo taarifa kuwa
halmashauri moja hapa nchini tayari imejipanga kupeleka madiwani wake kwenye
mafuzo na fedha watakazotumia ni za ruzuku ambazo serikali ya awamu ya
tano imeonya zisichezewe ovyo na badala yake zipelekwe kutatua changamoto za
wananchi.
"Ninapotoa gizo hili
hapa Geita natoa agizo kwa nchi nzima halmashauri zote ni marufuku, Mkurugenzi
atakaye thubutu kuchezea fedha ya ruzuku hatakuwa na kazi na mwenyekiti
atayefanya hivyo vilevile hatakuwa na kazi nitamwambia Rais afute halmashuri
hiyo,Nimewasikia watu wa Simiyu, wamepanga pesa ya ruzuku kwenda Kibaha
kwenye mafunzo washindwe na walegee ni marufuku kutumia fedha ya ruzuku
ya serikali iliyoletwa kwa ajili ya kutatua changamato za wananchi, sas
niseme halmashauri yoyote ambayo inataka kufanya hivyo ni lazima waombe kibali
kwangu lakini serikali ya Rais wetu John Magufuli haitaki semina ya kupeleka
Madiwani kujifunza namna ya kuvua samaki sijui ufugaji wa Nyuki”.Alisema
Simbachawene
Katika hatua nyingine Waziri
wa TAMISEMI amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Geita meja Jenerali Mstaafu Ezekiel
Kyunga na Katibu Tawala wa mkoa Selestine Gesimba, kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa fedha
zilizotengwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmashauri ya mji wa
Geita kwani inasemekana milioni 200 zimechezewa na wajanja.
“katika jengo la halmsahuri
mnalotaka kujenga zipo fedha zilizotolewa na Mgodi wa GGM bilioni 1.5 serikali
nayo imetoa Bilioni moja jumla mnazo bilioni 2.5 lakini ujenzi bado haujaanza
nimepewa taarifa katika fedha hizo Milioni 200 zimechezewwa na wajanja,Sasa
niagize Mhe. Mkuu Mkoa unavyo vyombo vyako vya ulinzi na usalama
hizo fedha zilizochezewa watuambie wamefanyia kazi gani na je ilipaswa iwe
hivyo?...maana jengo halipo mchoro wenyewe naambiwa hupo..agizo langu Mkuu wa
Mkoa na Ras natamani nipate zipo salama na kama hazipo salama tutaleteana
shida,’’aliagiza Simbachawene.
Ziara ya Waziri
Simbachawene Mkoani Geita, ilikuwa na lengo la kuzindua miradi, ambapo amezindua vyumba vya madarasa katika shule
nne za wilaya ya Geita na kwamba vyumba
hivyo vimegharimu zaidi ya Sh. Milioni 500 fedha kutoka serikali kuu program
for result (P4R) huku akitembelea mradi wa utengenezaji wa madawati katika
halmashauri ya wilaya hiyo.
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE
|
Post A Comment: