Usiku wa kuamkia leo mji wa Cairo
nchini Misri ulisimama dakika 90 kupisha pambano la mahasimu yaani
Derby iliyowakutanisha Zamalek ambao walikuwa wenyeji dhidi ya Al-Ahly
mchezo wa Ligi Kuu na kushuhudia wageni
wageni wakiibuka na ushindi wa
magoli 2-0.
Mchezo ulianza kwa ubabe kama
zinavyokuaga mechi za watani wengine haikuwachua muda Al-Ahly kupata
goli dakika ya 22 kupitia kwa mshambuliaji hatari mwenye uchu wa
kufumania nyavu,Moamen Zakaria baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Zamalek.
Licha ya kufungwa goli hilo
Zamalek waliendelea kufanya mashambulizi ya kushtukiza ili waweze
kusawazisha hata hivyo wageni walikuwa na ulinzi Imara hadi timu
zinakwenda mapumziko Al-Ahly walikuwa mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote kwa kucheza kwa umakini kupitia maelezo ya makocha wao huku
zikifanya mabadiliko ambayo hayakuweza kuwasaidia Zamalek kwani
walijikuta wakifungwa goli la pili dakika ya 90 kupitia kwa Junior Ajayi na kusababisha mashabiki wa Al-Ahly wakilipuka kwa shangwe.
Hadi dakika 90 mwamuzi anamaliza
Mpira Al-Ahly wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-0 na kujiweka
kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa mara ya pili.
Kwa matokeo hayo Al-Ahly
wamefikisha alama 45 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi
hiyo huku wakiwa wamecheza mechi 17 wakati wapinzani wao Zamalek wapo
katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 35 na kucheza mechi 15 wakiwa na
viporo viwili na Ligi hiyo itaendelea tena Leo kwa mechi tatu kupigwa.
Post A Comment: