MTOTO ADAIWA KUMUUWA BABA YAKE SINGIDA

Share it:




Mwenye tishert ya damu ya mzee ni Pius Malindisa ambaye ni mdogo wa marehemu



Jeshi la Mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa(29)mkazi wa mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano Manispaa ya Songea Mkoani humo kwa tuhuma za kumuua baba yake  mzazi Atanasi Malindisa [70] kwa kumpiga na kitu chenye ncha butu kichwani na kidevuni upande wa kushoto kisha kufanya jaribio la kuchimba shimo kwenye nyumba hiyo kwa malengo ya kumzikia baba huyo.

Akizungumza na Ruvuma TV katika eneo la tukio mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo wa marehemu Piusi Malindisa alisema kuwa wao walipata taarifa ya kifo cha ndugu yao Januari Mosi mwaka huu majira ya 1.30 kutoka kwa mtoto wa marehemu Patrck Malindisa .

Piusi alisema kuwa mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo na marehemu huyo alitoa taarifa kwa wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo na ndugu walipofika kabla ya kuingia chumbani alikokuwa akilala marehemu waliamua kuuita uongozi wa mtaa ambao uliingia na kubaini kuwa Atanasi Malindisa ameuwawa kwa kupigwa na kitu kichwani na kidevuni.

Alisema kuwa baada ya kubaini hilo walitoa taarifa polisi kisha mwili huo ulichukuliwa na kwenda kuuhifadhi Hospital ya mkoa Ruvuma [HOMSO] kwa uchunguzi huku jeshi la polisi likimshikilia mtoto wa marehemu kwa mahojiano zaidi.

Alifafanu kuwa polisi wakiwa bado kwenye nyumba hiyo walibaini kuwa kwenye moja ya chumba ambacho hakijaezekwa kulichimbwa shimo linaloendana na vipimo vya marehemu ambalo lilihisiwa kuwa alitaka amfukie humo ili watu wasijue kwa kuwa kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wawili.

“Uchimbaji wa shimo hilo lenye mithiri ya kaburi lilimshinda kisha akamua kulifukia na kuchukua hatua ya kuja kutoa taarifa kwetu wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo ambayo inadaiwa alikuwa akilia nalo kumbe sivyo bali kapigwa na kitu kichwani”alisema Ndugu wa marehemu.
Share it:

habari

matukio

Post A Comment: