Mkuu wa wilaya akiendelea kutoa maagizo juu ya taarifa iliyosomwa
Serikali ya Kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita
imetakiwa kupeleka taarifa yenye vielelezo kwa mkuu wa wilaya kuhusu matumizi
ya fedha kiasi cha shilingi milioni 51 katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vya
shule ya msingi Isingiro bila kufuata taratibu zilizokuwa zimewekwa
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya
Geita Mwl.Herman Kapufi kwenye mkutano
mkuu wa kijiji hicho baada ya wataalam wa hesabu za ndani katika Halmashauri ya
wilaya kutokubaliana na taarifa ya mtendaji wa kijiji hicho Bw. Samuel Shosha.
“Mwenyekiti wa serikali ya kijiji, mtendaji na
serikali yote ambao walikuwa wamepitisha mihtasali yote, Mkaguzi wa ndani,
kamati ya ulinzi na usalama tukutane ofisini kwangu tarehe mbili mwezi wa pili
muda wa saa tatu kamili lakini mwenyekiti wa kijiji unapokuja uje na mihtasali
yote,stakbadhi na nyaraka zote sitaki tena kisingizio lakini pia mnatakiwa mje
na daftari ambalo linaorodha ya mali zote zinazomilikiwa na
serikali”Alisisitiza Kapufi
Katika mkutano huo,Afisa mkaguzi wa ndani
Chacha Marwa amesema fedha zote za serikali zinatakiwa kuwa na vielelezo pamoja
na nyaraka zinazoainisha matumizi jambo ambalo halikuzingatiwa
Akifunga mkutano huo,mwenyekiti wa kijiji
Bw.Lumumba Salvatory amekanusha matumizi mabaya ya fedha hizo,huku akisema kuwa
hali hiyo inachochewa na Itikad za kisiasa ili kukwamisha jitihada za serikali
ya kijiji hicho.
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE
|
Post A Comment: