Waziri wa Mambo ya
Nje wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. Wang Yi akizungumza wakati wa kikao cha
majadiliano na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipofanya ziara ya siku
moja nchini leo jijini Dar es Salaam. Waziri huyo anatarajiwa kuondoka nchini
leo kuelekea DRC Congo kuendelea na ziara yake katika nchi za bara la Afrika.
Waziri wa Mambo ya Mambo ya Nje wa China, Wang
Yi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wao na
waandishi hao kufuatia ziara yake ya siku moja nchini. Kulia ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga
Baadhi ya
viongozi kutoka China na Tanzania
wakifuatilia mkutano baina ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Tanzania na
waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam. Miongoni mwao ni Balozi wa China
nchini Dkt. Lu Youqing( wapili kulia), Katibu MKuu Wizara ya Viwanda Biashara
na Uwekezaji, Dkt.Adelhelm
Meru.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipeana(kulia) mkono wa kheri na Waziri
wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya kumaliza kuongea na
waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China (walioshikana mikono) wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Tanzania na China mara
baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Post A Comment: