MAKONDA AAGIZA CHID MAPENZI KUKAMATWA ,MUME WA SHEMSA FORD

Share it:


Mume wa msanii wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford waliyefunga ndoa hivi karibuni, Chid Mapenzi ametajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba ni miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na kuagiza akakamatwe na polisi haraka iwezekanavyo.

Makonda ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar ambapo ametangaza kwamba anayo orodha nyingine ya watu 97 wanaotuhumiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.

Pia mtu mwingine aliyetajwa ni Ayubu Mfaume ambapo naye anatakiwa kukamatwa haraka iwezekanavyo.
Share it:

JOEL MADUKA

mastaa

Post A Comment:

Also Read

WANANCHI WALIA NA MKANDARASI WA BARABARA GEITA

Barabara inayotoka amerikani Chips Kuelekea Jimboni ikiwa kwenye hatua za awali za ujenzi. Mkuu wa mkoa wa Geita,Mh

JOEL MADUKA