NAPE AMKABIDHI RASMI OFISI WAZIRI MWAKYEMBE.

Share it:

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakikabidhiana hati za makabidhiano  rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe akimshukuru aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kwa kuitumikia Wizara kwa muda wote aliokuwepo.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakitia saini hati za makabidhiano  rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma akishubudia utiaji wa saini ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Prof Elisante Ole Gabriel .


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitoa neno kwa Waziri mpya na Waziri aliyepita wakati wa makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma.





Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye leo amekabidhi rasmi ofisi kwa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na watendaji wakuu wa Wizara, Mhe. Mwakyembe ameahidi kuwa licha ya kukabidhiwa ofisi, anaamini kuwa Mhe. Nnauye bado ni mdau mkubwa wa sekta za Wizara  na kuwa anategemea kuendelea kupata ushirikiano kutoka kwake.

Aidha Waziri Mwakyembe ameahidi kuendeleza yote mazuri yaliyo anzishwa na Mhe. Nnauye katika kuimarisha ufanisi wa Wizara na kuhakikisha inakuwa ni moja ya Wizara za mifano nchini. Amesisitiza kuwa katika kipindi kifupi alichokaa Wizarani, Mhe. Nnauye alianzisha mabadiliko makubwa na watu wameanza kuifahamu vizuri Wizara.

Kwa upande wake Mhe. Nnauye amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana kubwa ya kusimamia Wizara kwa kipindi cha miezi 15 huku akiwa ndio kwanza amekuwa mbunge katika awamu yake ya kwanza.Aidha Mhe. Nnauye ameahidi kuendela kushirikiana na Wizara kwa ukaribu kwani ni kweli yeye ni mdau mkubwa wa sekta za wizara hii.

“Heshima aliyonipa Mhe. Rais ni kubwa mno na nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini,” alisema Mhe. Nnauye. Aidha alisisitiza kuwa, tofauti na maneno ya mitandaoni, yeye atabaki kuwa mtiifu kwa Rais, Serikali na chama chake.

Pia amewashukuru watendaji wote wa Wizara kwa kumpa ushirikiano wa kutosha kwa kipindi chote alichofanya nao kazi na kuwaomba kutoa ushirikiano huo huo kwa Waziri wa sasa Mhe. Mwakyembe.



Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 10 MAY 2018

JOEL MADUKA