TANZIA: MWANDISHI WA HABARI CHANNEL TEN VALENCE ROBERT AFARIKI DUNIA

Share it:


Aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoa wa Geita,Vallence Robert Amefariki dunia Hii Leo Tarehe 28/03/2017, akiwa nyumbani kwao Muleba Kagera. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake Ribarikiwe..



Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Geita Daniel Limbe amethibitisha taarifa za kifo cha mwandishi wa habari Valence Robert.


Limbe ameiambia Maduka online  kuwa Valence Robert  hivi karibuni aliondoka mkoani Geita akiwa  anaumwa.


Hata hivyo inaelezwa kuwa Valence Robert alikuwa anaumwa ugonjwa usiojulikana.Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwao Misenyi.

Kwa mujibu wa Dada wa marehemu  Angela Robart  ameiambia Maduka online kuwa mazishi yatafanyika siku ya Alhamisi tarehe 30 majira ya saa Tisa mchana.



Hivi karibuni Valence Robert na Joel Maduka walipigwa na askari polisi wakati wakiwatawanya wananchi kwenye maeneo ya stendi ya zamani Mjini Geita ambao walikusanyika kusalimiana na Waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Taifa ya  Chadema Edward Lowassa.



Share it:

JOEL MADUKA

TANZIA

Post A Comment:

Also Read

ASKOFU WA AIC NCHI AHAIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KWENYE NYANJA ZA KIJAMII

JOEL MADUKA