Wananchi wa mtaa wa Nyantorontoro "A"Kata ya Nyankumbu wakikwa kwenye shughuli ya kujitolea ya utengenezaji wa Barabara. |
Shule ya Msingi ambayo wananchi wamejitolea kutengeneza Barabara ya kufika shuleni Hapo. |
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyantorontoro Gerevas Kayelelo kulia akifokeana na moja kati ya wananchi ambaye hakutaka eneo lake kuondolewa mihogo ambayo alikuwa amepanda. |
Elias Totoe mkazi wa nyantorotoro akizungumza namna ambavyo wameweza kufikia uwamuzi wa kutoa maeneo yao kwaajili ya maendeleo ya mitaa.
|
Lecta Maningu mkazi nyantorotoro akieleza juu ya tatizo la maji ambavyo limekuwa ni changamoto katika kata hiyo. |
Wananchi wakionesha vitendea kazi |
Gerevas Kayelelo m/kiti mtaa wa Nyantorotoro A,akifafanua juu ya uwamuzi wa wananchi kujitokeza kwenye shughuli ya utengenezaji wa barabara. |
Barabara ni
moja Kati ya huduma muhimu za kijamii zinazohitajika ili kuchochea kasi ya maendeleo
lakini maeneo yaliyo mengi hususani kwenye mitaa kumekuwepo na changamoto ya miundombinu hiyo ambayo
inarahisisha kasi ya maaendeleo.
Kutokana na
hali hiyo wananchi wa mtaa wa nyantorotoro “A”
kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita wamejitokeza kutengeneza barabara ya kiwango cha molamu yenye kilomita zipatazo mbili kuelekea kwenye
taasisi ya shule mpya ya mtaa huo.
Baadhi ya wananchi wamezungumza na mtandao wa Maduka
Online na kwamba wamejitolea kutengeneza Barabara kwa ushirikiano ni kutokana na muda
mrefu kutokuwepo kwa barabara na shule kwenye mtaa huo.
“Kiukweli
watoto wetu wamepata shida kwa muda mrefu na kusoma umbali wa kilomita nyingi
kutokana na shule kukamilika tumeonelea basi sisi pamoja na mwenyekiti wetu wa
mtaa kuweka jitihada za kutengeneza barabara ambayo itaelekea shuleni na
itawasaidia watoto wetu kutembea kwa ukaribu kufuata elimu”alisema Lecta
Maningu.
“Pamoja na kwamba sisi kama wananchi
tumejitolea kujenga barabara ambayo inaelekea shuleni lakini tunaiomba serikali
yetu kupitia kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji kuona umuhimu wa kuweka maji
shuleni hapo ili kupunguza adha kwa wanafunzi shuleni hapo kwani hakuna maji”aliomba
Bi, Cesilia Clement
Lakini
pamoja na baadhi ya wananchi kutoa
maeneo yao kwa hiyari ili kupitisha
barabara, wapo wengine wanakwamisha juhudi za wengi kufikia malengo hayo, kama
mzee aliyetambulika kwa jina la Mayenga
ambaye ameonekana mgumu wa kutoa eneo lake lililolimwa mihogo jambo ambalo
limesababisha malumbano makali baina
yake na wananchi.
Mwenyekiti
wa Mtaa huo Gerevas Kayelelo, alisema kuwa wananchi wake wametoa ardhi yao kwa
ajili ya barabara bila kuomba hata fidia ya aina yoyote.
Pamoja na kutokuwa na muafaka baadhi ya wananchi wamelalamikia kitendo cha Bw Mayenge kuwa ni moja Kati ya watu ambao wanaonekana kukwamisha juhudi za serikali za mtaa huo za kujitolea kuleta maendeleo ya mtaa huku wakimwomba mwenyekiti wao kuliangalia hilo kwa umakini kwani baadhi ya watu wametoa maeneo yao kwa hiyari na ni kwanini mtu mmoja hakwamishe jitihada za watu Wengi.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: