Mkuu wa mkoa wa Kagera ,Meja jenerali Mstaafu,Salum Kijuu akisoma taarifa ya miradi ambayo itapitiwa na mwenge wa uhuru.
Mwenge wa
uhuru umeliza mbio zake Mkoani Geita na kukabidhiwa mkoa wa Kagera huku miradi mitano ikishindwa
kuzinduliwa kutokana na taarifa ya gharama za miradi hiyo kutofautiana na ya
Mkoa.
Akisoma taarifa ya shughuli za mbio za mwenge wa
uhuru zilivyofanyika Mkoani Humo,Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert
Gabriel amesema jumla ya miradi sitini na tatu yenye thamini ya
sh ,bilioni 12.7 imepitiwa na mwenge wa
uhuru huku mitano ikishindwa kuzinduliwa
serikali ikiendelea na uchunguzi kubaini tatizo la miradi ambayo
haikuzinduliwa na kwamba tayari TAKUKURU
wamekiwisha kuagizwa kufanya uchunguzi wa kina kwenye miradi hiyo.
Sanjali na hayo Mhandisi Robert Gabriel ameelezea
mmomonyoko wa maadili ambavyo umeendelea
kulikumba Taifa na kwamba kupitia mbio hizo awana budu kuendelea kukemea na
kulaani vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiwaelemea zaidi vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
Aidha Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa ,Charles Kabeho amempongeza Mkuu wa
Mkoa wa Geita kwa namna ambavyo wameweza kutumia fedha za lipa kutokana na
matokeo sasa kwa kujenga majengo mazuri
ya madarasa kwa Bei nafuu Zaidi.
Mkuu wa mkoa
wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu amesema miradi ambayo itapitiwa na mwenge wa uhuru ni 80 na thamani yake ni bilioni 11 na
halmashauri nane ndizo ambazo zitapitiwa.
Mwenge wa uhuru umeanza mbio zake leo Mkoani Kagera ambapo utakimbizwa
kwenye halmashauri nane huku
kauli mbiu ikiwa ni elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya
Taifa letu.
|
Post A Comment: