RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli leo Septemba 7, 2017 amepokea ripoti za uchunguzi wa madini ya
Tanzanite na Almasi kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
zilizotokana na kamati mbili (Kamati ya Tanzanite iliongozwa na
Mwenyekiti Dotto Biteko na Kamati ya Almas ilikuwa chini ya Mwenyekiti
Mussa Azzan Zungu) zilizoundwa na spika wa Bunge, Job Ndugai . Muda
mfupi baada ya kupokea ripoti hizo, Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa
ametengua uteuzi wa wateule wote waliotajwa katika ripoti hizo.
Miongoni mwa wateule wa Rais waliotajwa katika ripoti hiyo
ni pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene,
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Edwin Ngonyani. Wengine waliotajwa
katika taarifa hizo ni pamoja na Katibu Tawala Eliakim Maswi, wabunge
Willium Ngeleja na Andrew Chenge.
Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kupikea ripoti hiyo,
Rais Dkt. Magufuli alisema “uwe RC,Waziri wau Mkurugenzi na umetajwa
kwenye ripoti ya uchunguzi hauwezi kuendelea na wewe upo kwenye
Serikali, Utupishe”.
“Kuna baadhi ya wabunge kama ulivyosema mheshimiwa Spika,
kila mahali yupo, katika kashfa fulani yupo, katika hili yupo, katika
lile yupo. Tena wengine bado wapo bungeni na wakati mwingine wanachangia
mpaka mishipa inawatoka, taratibu zifanyike kuwachukulia hatua” Rais
Magufuli Rais Magufuli amewasifu watanzania wazalendo ambao wako tayari
kutoa uhai wao kwa ajili ya Taifa lao.
“Tunawatumia watanzania wazalendo kupata taarifa za
kizalendo kwa Taifa letu, wapo watanzania wanaorubuniwa na kuisaliti
nchi yao, hao hawafai” Rais Dk John Pombe Magufuli, Ikulu. Dar es
Salaam.
Katika maelezo yake kabla ya kumkabidhi Rais ripoti hizo,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kwa muda mrefu watanzania wamekuwa
wakilalamika serikali kutowajali na kuwasikiliza. Amesema kupitia
serikali ya Awamu ya Tano sasa watanzania wote watakuwa na haki sawa na
wote watasikilizwa.
“Watanzania ambao kwa miaka mingi wamejihisi hawasikilizwi
na hawahurumiwi sasa ni wakati wao kujihisi kuwa ni watanzania na
wanastahili haki zote kama watanzania kupitia serikali yako mheshimiwa
Rais” Kassim Majaliwa
Rais Magufuli amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa ripoti hizo za madini kwa ajili ya kufanyiwa kazi mara moja.
CHANZO/FULL SHANGWE.
Post A Comment: