RAIS DK SHEIN ALIPOWAAPISHA WAKUU WA VIKOSI VYA JKU NA CHUO CHA MAFUNZO

Share it:
 

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                              13.06.2017
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Viongozi wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), aliowateua hivi karibuni kuwa Wakuu katika Vikosi hivyo.

Katika hafla hiyo, Dk. Shein kabla ya kumuapisha Naibu Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Ali Abdalla Ali, alimfisha cheo cha Ukamishna na baadae kumuapisha kuwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo, Zanzibar.

Wakati huo huo, Dk. Shein, amemuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU).

Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za (SMZ), Haji Omar Kheir, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.

Wengine ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,  Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
Share it:

IKULU

Post A Comment: