RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Share it:
.
KID3
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akiwa na Katibu Tawala Mkoa, Albert Msovela (katikati) pamoja na Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese (kushoto) wakati wa ziara.
KID4
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga.
KID5
Mjasirimalia Mabela Msolwa kutoka wilayani Kishapu akitoa maelezo kuhusu mradi wake wa mashine za kuchakata nafaka na ghala  kuhifdhi nafaka kwa Mkuu wa mkoa (kulia) na viongozi wengine wakati wa ziara hiyo.
KID6
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kishapu, Lucas Said (kushoto) akitoa maelezo kuhusu mradi wa huduma ya maji ya Ziwa Victoria kwa wananchi kata ya Maganzo.
KID7
 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akitoa maelekezo wakati alipotembelea ghala la nafaka la Mabela mjini Mhunze kata ya Kishapu wakati wa ziara yake.
KID8
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akifafanua jambo kwa viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo kijiji cha Kinampanda kata ya Mwamalasa.

Na Robert Hokororo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika ziara hiyo Telack alikagua mradi wa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria uliopo kata ya Maganzo na maendeleo ya ujenzi wa zahanati kata ya Shagihilu.
Mradi mwingine ni wa mjasiriamali wa kusindika alizeti na kukoboa nafaka za mpunga na mahindi ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Kwenye kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea mradi mwingine wa ghala la kuhifadhi nafaka na mashine za kukoboa nafaka za mahindi na mpunga.
Katika ziara hiyo kiongozi huyo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa was Shinyanga, Muliro Jumanne Muliro.
Alikaribishwa na mwenyeji wake, Mkuu wa wilaya, Nyabaganga Talaba, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya na wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.
Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUWEKEZA KWENYE ELIMU GEITA

JOEL MADUKA