![]() |
Waziri wa maji na Umwagiliaji Gerson Lwenye alipokuwa akikagaua baadhi ya mitambo itakayotumika kusukuma maji katika chujio la maji katika bwawa la New sola kijiji cha Zanzui mwezi march.
|
![]() |
Matanki ya maji katika kijiji cha Zanzui ambapo awali yalikuwa yakitoa maji machafu kwenda kwa wananchi.
(PICHA ZOTE Na Maktaba ya COSTANTINE MATHIAS-SIMIYU).
|
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
AGIZO la Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge alilolitoa mwezi machi kutaka chujio la Maji katika bwawa la New Sola lililoko katika kijiji cha Zanzui wilayani Maswa mkoani Simiyu liwe limekamilika kufikia juni 30 mwaka huu limeshindwa kutekelezwa.
Lwenge alitoa agizo hilo Februari 19 mwaka huu alipofanya ziara yake mkoani hapa na kukagua ujenzi wa chujio hilo unaofanywa na Mkandarasi Kampuni ya Pety Co-operation Ltd anayeshirikina na kampuni ya Josam Company Ltd zote za mjini Kahama mkoani Shinyanga mara kwa mara kuomba kuongeza na kupewa muda wa kukamilisha ujenzi wa mradi huo.
Mkandarasi huyo alimwomba Waziri kumwongezea siku 132 ili aweze kukamilisha ujenzi wa chujio hilo ambapo zimemalizika juni 30 mwaka huu lakini ujenzi huo haujakamilika hadi sasa.
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari umebaini ya kuwa hadi sasa ujenzi huo haujakamilika na hivyo kufanya kuwa kero kubwa na kusababisha wananchi wa mji wa Maswa na vijiji 11 kukosa maji ya baada ya chujio hilo kuharibika na kushindwa kuyaelewa maagizo ya waziri huyo kama vile yalikuwa ya kujifurahisha au ya kisiasa.
Uchunguzi huo umebaini ya kuwa hadi sasa wananchi wa maeneo hayo wanaotumia maji hayo wamekuwa wakilalamika kuwa yamekuwa na kiwango kikubwa cha uchafu (tope) huku wakiendelea kulipia ankra za maji kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (Mauwasa).
Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa, Mhandisi Merchades Anaclet akizungumzia ujenzi huo alisema kuwa hadi sasa ni ujenzi wa chujio hilo kwa sasa ni asilimia 68 kusisitiza kuwa agizo alilolitoa Waziri wa Maji limeshindwa kutekelezwa kwa wakati.
“Mradi wa ujenzi wa chujio katika chanzo chetu kikuu cha maji katika bwawa la New Sola lililoko katika kijiji cha Zanzui kwa sasa ni asilimia 68 na hivyo kuwa nyuma ya lile agizo la Waziri alilomtaka mkandarasi kukamilisha kufikia juni 30 mwaka huu na Mradi huu unasimamiwa na Wizara moja kwa moja na si Mamlaka yetu,”alisema.
Katika ziara hiyo aliyoifanya Waziri alimwonya na kumtahadharisha Mkandarasi ya kuwa endapo hata kamilisha ujenzi wa chujio hilo kwa mujibu wa mkataba aliopewa atakuwa katika jopo la wakandarasi watakao kosa sifa za kupata kazi popote hapa nchini.
Aidha alisema na kuonya kuwa kushindwa kukamilika kwa ujenzi wa chujio hilo kutakuwa kuna muweka mahali pabaya mkandarasi huyo kuendelea kupata kandarasi zingine hapa nchi.
Kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa chujio hilo ulianza agosti mwaka juzi na unaogharimu Sh bilioni 3.5 uliotarajiwa kukamilika machi 31 mwaka huu kumeathiri wananchi wa mji wa Maswa na vijiji 11 sasa kutumia maji yasiyo chujwa na kuwa katika hatari ya kupata magonjwa yatokanayo na maji ikiwemo homa za matumbo,kuharisha na hata kipindupindu.
Licha ya wananchi wa mji wa Maswa kukumbwa na adha hiyo pia wananchi wa vijiji vya Dodoma,Zanzui, Malita, Mwabayanda, Hinduki, Mwadila, Buyubi, Mwasita, Mwingwa, Iyogola na Badabada wameathirika na kutokamilika kwa chujio hilo.
Post A Comment: