MTOTO WA MIAKA MINANE AFANYIWA UKATILI KWA KUCHOMWA NA KIJIKO CHA MOTO GEITA

Share it:
Mtoto huyo akionesha majeraha ya kuchomwa na kijiko ambacho kilikuwa kimepashwa moto maeneo ya miguuni.

Jeraha la Masikioni ambalo na lenyewe alichomwa na mama wa Kambo.


Bi,Benitha Agustine  ambaye ni mama wa Kufikia wa Mtoto ambaye amekuwa akimfanyia ukatili.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Esnath Magoti  akizungumzia matukio ya ukatili ambayo yapo Mkoani Humo.




Vitendo vya ukatili dhidi  ya watoto bado vimeendelea kushamiri Mkoani Geita ambapo Kuanzia mwezi Januari hadi  Juni mwaka Huu Jumla  ya makosa ya vitendo vya ukatili dhidi ya  watoto  mia moja Tisini na Tisa (199) vimekwisha ripotiwa kwenye dawati la Jinsia na Watoto.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye  ofisi za polisi Mkoani Humo,Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Esnath Magoti ,amefafanua kuwa  mchanganuo wa Makosa hayo ni kesi za ubakaji,ulawiti ,watoto kutelekezwa ,wengine kutokuwapeleka shule na vitendo vingine vya ukatili dhidi ya watoto.

“Unyanyasaji  wa Kijinsia bado  ni tatizo kubwa sana kwenye Mkoa wetu wa Geita kwani hadi sasa Jumla ya Kesi mia moja Tisini na Tisa (199) zimekwisha Kufika kwenye meza yetu na kesi nyingi unakuta ni za ubakaji ,ulawiti na wengine wanatenda ukatili wa kuwadhuru watoto mara nyingi kesi hizi zinakwama kutokana na jamii kushindwa kuwa na ushirikiano kwa kutoa taarifa wengine wamekuwa wakimalizana wao kwa wao kwenye familia zao hali hii inakwamisha sana jitihada za utetezi wa watoto ambao wanafanyiwa vitendo vya ukatili”Alisema Magoti.

Hata hivyo kutokana  na juhudi za utoaji wa elimu juu ya watu kuachana na vitendo vya ukatili hali bado sio swari ambapo kwenye mtaa wa Msalala Road kata ya Kalangalala,Mama wa kufikia  ambaye anajulikana kwa jina la Benitha Augustine,amemchoma  mtoto mwenye umri wa miaka minane (8)  sehemu mbali mbali za mwili wake na kijiko ambacho alikuwa amekipasha moto kwa madai kuwa alikuwa akimhadhibu .

Akizungumza na Mtandao wa Maduka Online Jirani wa Mama Huyo Bi,Habiba Rajabu alisema kuwa Mama Huyo amekuwa na tabia ya kumpiga mara kwa mara mtoto huyo bila sababu hali ambayo wao kama majirani wamekuwa wakijiuliza labda kwasababu sio mtoto wake wa kuzaa ndio maana amekuwa akimsulubu kwa mateso ya namna hiyo.

 “Sisi kama majirani tumeendelea kumshauri kama mtoto amemshinda ni bora akampeleka kwa mama yake kuliko kuendelea kumfanyia vitendo vya ukatili wa  namna hiyo amefikia hatua hadi anamchoma na kijiko ambacho amekipasha moto kiukweli inaumaa sana kwa mtoto ambaye ni kiumbe wa Mungu kufanyiwa ukatili wa namna hii yani hadi na baba yake mzazi ana mapenzi na mtoto ukimkuta anamwadhibu utadhani anaadhibu jambazi jamani watu tubadilike ukatili wa jinsi hii haukubaliki kwenye jamii zetu”Alisema Bi Habiba.

Aidha mama Huyo Bi,Benitha Agustine amekiri kufanya kitendo cha kumpiga mwanae na kumchoma kwa kutumia kijiko ambacho amekichemsha kwenye moto na kwamba amekuwa akifanya hivyo kutokana na hasira ambazo zinasababishwa na ugomvi baina yake na mume wake kwani amekuwa akimpiga mara kwa mara hali ambayo imekuwa ikipelekea kupatwa na hasira ambazo zimekuwa zinapelekea kumwadhibu mtoto wake.

 Kutokana na kufanyiwa ukatili huo Mtoto huyo   ameiomba serikali kumchukulia hatua za kisheria mama yake wa kambo kwani imekuwa ni destulri yake kumtesa kwa muda mrefu hali ambayo imemsababishia kuwa na majeraha sehemu nyingi za mwili wake.

Shida Mpondi ni Katibu wa Mbunge wa viti maalum Chadema Mkoani Hapa ametoa wito kwa wazazi,walenzi na baadhi ya watu wenye tabia za namna hiyo kuachana nazo kwani zinawakosesha haki za msingi watoto na kuwafanya kudumaa kiakili.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

Share it:

JOEL MADUKA

matukio

Post A Comment:

Also Read

JUMIA KUWAWEZESHA WATANZANIA KUMILIKI SIMU ZA KISASA KWA BEI NAFUU

Yapunguza bei za simu mpaka 60%! Mteja kuunganishwa na kifurushi cha internet ya bure kutoka Tigo mpaka GB 18 

JOEL MADUKA