Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medard Kalemani
amewaagiza Mameneja wa Tanesco wilaya na mikoa yote nchini kuweka madawati kwa
ajili ya kuwahudumia wananchi walio mbali na ofisi za Tanesco hususani maeneo
ya viijijini.
Amesema wananchi wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata
huduma hivyo ni vyema wataalam, meneja na wakurugenzi wakawafuata wateja walipo
maeneo ya mbali badala ya kusubiri wafuatwe ofisini.
“ Na hili ni agizo ninalitoa kwa nchi nzima mameneja wa Tanesco Ngazi ya
Wilaya na Mikoa wekeni dawati kwenye maeneo ambayo hayana ofisi za tanesco ”Alisisitiza
Kalemani.
Dk Kalemani pia amewasisitiza wakandarasi wa Shirika la
White City International kutumia miezi
16 kusambaza Umeme kwenye vijiji 220
walivyopatiwa mkoani Geita.
Meneja Utaalamu Elekezi wa REA, Mhandisi Gissima Nyamo-hanga
amesema katika mradi wa huduma ya umeme vijijini, Serikali imetenga Sh Bilioni
78.56 kwa ajili ya kusambaza umeme mkoani Geita na kuwataka wananchi wawe
makini na watu wanaoweza kuwalaghai
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: